Posts

RUSHWA MUHALI BADO NI TATIZO KWA JAMII

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA. Imebanika kuwa  rushwa  muhali  bado  ni  kilio  kikubwa  kinachoendelea  kuikumba  jamii  hali ambayo  inapelekea   kesi  nyingi  za  udhalilishaji  kufutwa  Mahakamani  kutokana  na kukosa  ushahidi. Wakizungumza  katika mkutano  wa  robo mwaka wa kujadili juu  ya  utekelezaji  wa  majukumu yao wana mtandao  wa kupinga udhalilishaji kutoka  wilaya  ya  Mkoani huko  ukumbi wa Chama cha Wandishi  wa habari Wanawake Tanzania [Tamwa] iliyopo chake chake Pemba. Wamesema licha ya juhudi  zinazoendelea  kuchukuliwa na Serikali pamoja na wanaharakati mbali mbali  ya kuwafahamisha jamii kufahamu  madhara ya udhalilishaji lakini bado juhudi hizo zinagonga mwamba. Wamesema  wamebaini kuwa  wengi wafanyaji  wa matukio hayo huwa ni ndugu wa familia  moja, hivyo h...

ANAYEDAIWA KUMLAWITI MTU MWENYE ULEMAVU WA AKILI PEMBA, APATA UZIWI GHAFLA MAHAKAMANI

NA FATMA HAMAD, PEMBA HAKIMU wa mahakama Mkoa Wete, Mwendesha mashtaka, Karani, na askari wa mahakama, wamepigwa na butwaa baada ya baba mzazi wa mtuhumiwa wa ulawiti, kudai mtoto wake ni kiziwi. Awali mtuhumiwa huyo alikuwa ni mzungumzaji mzuri, wakati kesi yake ikiendeshwa mahakamani hapo kabla ya kuondolewa kwa madai ya kudanganya umri. Ilibainika kuwa wazazi wa kijana huyo mwenye miaka 19, anaedaiwa kumlawiti kijana mwenzake mwenye ulemavu wa akili na kisha kupandishwa katika mahakama ya mkoa B Wete, Febuari 13, mwaka huu ingawa kesi yake iliondolewa mwezi Machi mwaka huu baada ya kudaiwa kudanganya umri. Ndipo mahakama ya mkoa ‘B’ ilipompandisha kwenye kizimba chake na kusomewa upya shtaka lake, kama mtu mzima, ingawa baba mzazi kabla ya mtoto wake [mtuhumiwa] kujibu lolote, alidai kuwa ni kiziwi. Hoja ya mzazi huyo, ilichukua takriban dakika mbili mahakamani hapo, ikijadiliwa baina ya hakimu, mwendesha mashtaka na baba mzazi, juu ya ulemavu ulioibuka ghafla na kuwashang...

WALIMU WA MADRASA WAENDELEZA VIPAJI VYA QUR AN

Image
Walimu wa madrasa za Qurani   pamoja   na wazazi   wametakiwa kushirikiana kwa    pamoja   kuwasimamia   watoto   wao   kuhakikisha   wanaendeleza    suala la uhifadhi wa Qurani     ili kupatikana vipaji   vyenye ubora. Hayo yamesemwa na Mmoja wa wazazi   wa wanafunzi   wa madarasa za kurana   Ali Hamad Bakari   katika hafla ya mashindano ya tahfidh lkuran yaliofanyika Viwanja vya mpira Pwepweu viliopo   Tumbe wilaya ya Micheweni Mkoa waKaskazini Pemba   amesema uhifadhi wa kurani ni suala muhimu kwani hupelekea   kuwepo   na kizazi   chenye   madili. ‘’Mashirikiano ya pamoja ndio njia pekee inayopelekea wanafunzi kuendeleza masomo yao na kuibua vipaji’’ alieleza mzazi. Akitoa nasaha zake mara   bada ya kumalizika kwa mashindano hayo Msaidizi   wa Katibu   mtendaji Ofisi ya Mufti mkuu upande wa Pemba Said Ahmad amewawataka walimu wa madrasa ...

NUHU KOMBO NUHU AENDELEA KUSOTA RUMANDE

Image
  NA FATMA HAMAD-- PEMBA. Hatimae mahakama ya mkoa B Wete, imemrejesha tena rumande mtuhumiwa wa ulawiti Kombo Nuhu Kombo miaka 19 baada ya kubainika kuwa ni mtu mzima licha ya awali kupewa dhamana kama ni mtoto mahakamani hapo. Awali mtuhumiwa alipelekwa rumande mwanzoni mwa mwaka huu kwa tuhuma za ulawiti kwa kijana mwenye ulemavu wa akili ingawa upande wa utetezi ulidai na kuthibitisha kuwa mteja wao hakutendewa haki kupelekwa rumande kwa sababu ni mtoto. Wakati kesi yake ikiendelea miezi mitatu iliyopita   na kuwasilishwa   vielelezo mahakamani hapo na upande wa utetezi mahakamani   iliridhia na kumpa dhamana mtuhumiwa huyo   kama mtoto. Huku upande wa mashtaka ukiendelea kung’ang’ania   kwamba mtuhumiwa ni mtu mzima, kisha uliwasilisha vielelezo kadhaa ikiwemo cheti cha kuzaliwa cha mtuhumiwa na mahakama kutengua uwamuzi wake wa awali juu ya umri wa mtuhumiwa. Mwendewsha mashtaka katika shauri hilo Juma Ali Juma alidai mahakamani hapo kuwa an...

UDHALILISHAJI BADO NI KILIO KWA WANAWAKE NA WATOTO

Image
  NA FATMA HAMAD- PEMBA. Mahakama   maalum inayoshughulikia kesi za udhalilishaji mkoa wa Kusini Pemba imeihairisha kesi ya ubakaji inayomkabili mtuhumiwa Ali Usi Simai mtumzima wa miaka 32 mkaazi wa Mchakwe Muambe anaedaiwa kumbaka msichana wa   miaka   nane (8)ambapo kufanya hivyo ni kosa kisheria. Akizungumza mbele ya Mahakama hiyo mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya mkurugenzi   wa mashtaka DPP   Seif Mohd Khamis ,aliiambia mahakama   iihairishe kesi hiyo   kwani   upande wa mashtaka hawakupokea   chaji shiti   ya kesi wenyewe. “Mheshimiwa sikupokea chaji shiti, kwa hivyo siwezi kucheza na haki ya mtu   kwani sijui kilichoandikwa kwenye file hilo naomba uipangie siku nyengine ili niweze kulipitia’’, alisema DPP Seif. Kwa upande wake wakili wa kujitegemea Saleh Said Moh’d alisema hakubaliani na ombi hilo kwani   wamekuja na mashahidi 4 akiwemo   mwenyewe   mtuhumiwa, hivyo kuihairisha itakuw...

KUKOSEKANA MKALIMANI MASKULINI BADO NI TATIZO KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU

Image
  NA FATMA HAMAD-- PEMBA. Kukosekana kwa walimu wanaojua lugha za alama maskulini bado ni kilio kikubwa kinacho wa kwaza wanafunzi wenye ulemavu kisiwani Pemba. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Kwale gongo wilaya ya Wete kaskazini Pemba, wazazi wa watoto wenye ulemavu walisema suala la kuchanganywa darasa   pamoja na wanafunzi wengine bila ya kuepo kwa   mwalimu wa lugha za alama kunachangia wanafunzi hao kutofaulu mitihani yao na kusababisha kushindwa kufikia malengo yao. ‘’Mfumo wa elimu mjumuishi wa kuchanganywa pamoja na wanafunzi wenye ulemavu na   wengine   bado hauja watendea haki watu wa aina hiyo   maskulini,’’ alisema mama mzazi wa Abdala Hussein mwenye ulemavu wa uziwi, mdomo na mguu. Alisema mtoto wake anasoma darasa la kumi ila hana tamaa ya kufaulu kutokana na changamoto hiyo   na kuiomba   wizara ya elimu kumuona   kijana huyo na kuweza kumsaidia kwa hali na mali ili kuona na yeye amekuja na u...

Kukosekana kwa mkalimani maskulini kunadumaza mafanikio ya wanafunzi wenye ulemavu Pemba

Image
  NA FATMA HAMAD-- PEMBA. Kukosekana kwa walimu wanaojua lugha za alama maskulini bado ni kilio kikubwa kinacho wa kwaza wanafunziwenyeulemavu kisiwani Pemba. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Kwale gongo wilaya ya Wete kaskazini Pemba, wazazi wa watoto wenye ulemavu walisema suala la kuchanganywa darasa  pamoja na wanafunzi wengine bila ya kuepo kwa  mwalimu wa lugha za alama kunachangia wanafunzi hao kutofaulu mitihani yao na kusababisha kushindwa kufikia malengo yao. ‘’Mfumo wa elimu mjumuishi wa kuchanganywa pamoja na wanafunzi wenye ulemavu na  wengine  bado hauja watendea haki watu wa aina hiyo  maskulini,’’ alisema mama mzazi wa Abdala Hussein mwenye ulemavu wa uziwi, mdomo na mguu. Alisema mtoto wake anasoma darasa la kumi ila hana tamaa ya kufaulu kutokana na changamoto hiyo  na kuiomba  wizara ya elimu kumuona  kijana huyo na kuweza kumsaidia kwa hali na mali ili kuona na yeye amekuja na ufaulu mzur...