Posts

Showing posts from October, 2020

UBAKAJI BADO NI TATIZO

Image
  Mahakamayamkoachakechakeimeiondoshakesiyaubakajiinayowakabili habibrashidkhamis mwenyeumriwa 25 mkaaziwakungenipamojana yassirabdalakhamis mwenyeumri 19 mkaaziwashungiwilayachakemkoawakusinipemba baada yay a mtuhumiwahabibu Rashid kuthibitikakuwaameshafungandoanamsichanawamiaka 16. UwamuzihuoumekujabaadayaMwendeshamashtakawaserikalikutokaofisiyamkurugenziwamashtakajumaalijumakuithibitishiaMahakamakuwatayarimtuhumiwanambambiliameshafungaNdoanaMtotoanaedaiwakumbaka. Mwendeshamashtakawaserikalikutokaofisiyamkurugenziwamashtakajumaalijumaaliambiamahakamahiyokuwamtuhumiwahabiburashidtayariameshafunganaendoamsichanahuyo , nasasawanaishipamojakimumenamkenahivyohakunatenakesiitakayoendeleanakupatikanakwaushahidihalisi. HivyoHakimuwaMahakamahiyolusianoMakoeNyengoalipokubaliananaombila upandewamashtakanakutangazarasmikuliondoshashaurihilo la tuhumazaUtorashajinaubakaji. ImedaiwaMahakamanihapowatuhumiwahaowalifanyaMakosamawilitofautiambapokosa la kwanza sikuisiyofahamikamweziwa 7 mwakahuusa 1;

Shahidi amuweka mataani Mtuhumiwa

Image
  KUTOKUWEPO KWA SHAHIDI  KUMEPELEKEA  HAKIMU WA MAHAKAMA YA MKOA  CHAKE CHAKE  LUSIANO MAKOE NYENGO  KUGHAIRISHA KESI YA UBAKAJI INAYOMKABILI MTUHUMIWA HAJI HAMAD HAIDAR MWENYE UMRI WA MIAKA 30 MKAAZI WA GOMBANI CHAKE CHAKE PEMBA. MWENDESHA MASHTAKA  WA SERIKALI  JUMA ALI JUMA ALIAMBIA MAHAKAMA HIYO KUWA KESI HIYO IKOKWAAJILI Ya KUSIKILIZA USHAHIDI. AMEDAI KUWA SHAURI HILO LA UBAKAJI KUMPOKEA SHAHIDI AMBAE NI DAKTARI INGAWA HAKUWEZA KUFIKA KUTOKANA  NA KUWEPO KATIKA LIKIZO. ‘’LEO TULITARAJIA KUPOKEA SHAIDI AMBAE NI DAKTARI LAKINI HAKUWEZA KUFIKA HIVYO TUNAIOMBA MAHAKAMA YAKO IPANGE SIKUNYENGINE KWA AJILI YA KUSIKILIZWA. HAKIMU WA MAHAKAMA HIYO LUSIANO MAKOE NYENGO ALIKUBALIANA NA OMBI LA UPANDE WA MASHTAKA NA KULITAKA SHAURI HILO LIRUDITENA DESEMBA 8 MWAKA HUU. IMEDAIWA MAHAKAMANI HAPO SIKU YA TAREHE 16/8/2019 MAJIRA NYA SA 6; MCHANA HUKO GOMBANI WILAYA YA CHAKE CHAKE ALIMBAKA MSICHANA MWENYE UMRI WA 15 , AMBAPO KUFANYA HIVYO NI KOSA KINYUME NA KIFUNGU CHA 108 [1] [2] [e] na

Aendelea kusota Rumande kwa tuhuma za Ubakaji

Image
  Mtuhumiwa Bakar Mbwana Juma mwenye umri wa miaka 32 mkaazi wa Jomvu Kengeja anaekabiliwa na shitaka la Kumtorosha na Kumbaka msichana mwenye umri wa 17 ameiambia mahakama ya Mkoa Chake Chake kuwa yeye hahusiki na tukio hilo kwani muda uliotajwa kutenda kosa hilo alikua kwenye kibanda akinywa kahawa. Aliambia mahakama hiyo kuwa yeye ni mfanya kazi wa ujenzi wa nyumba hivyo anakawaida ya kurudi kazini   baina ya saa moja hadi saa moja na nusu za usiku na mara zote hufikia kwenye mkahawa kabla ya kwenda anakoishi. Alidai kuwa siku ambayo alituhumiwa kufanya tukio hilo alirudi kazini majira ya moja za usiku na kifikia mgahawani na kupata kahawa akiwa yeye na marafiki zake. Alifahamisha kuwa baada ya kunywa kahawa alirudi nyumbani na kuigia chooni kwa ajili kujiandaa na sala ya Isha na kisha kwenda msikitini.   ‘’Nashangaa sana  wakati huo wa saa mbili nitatorosha saa ngapi na nitabaka saa ngapi hilo haliwezekani’’ Alidai mtuhumiwa huyo. Alidai kuwa kabla ya kutokea kwa tukio  h

Bidhaa zenye Viwango ndio chanzo cha maendeleo kwa Wajasiriamali.

Image
  Wajasiriamali Kisiwani   wametakiwa   kuzalisha Bidhaa   zenye   ubora na zenye   Viwango   ili kupata Soko la ndani na nje ya Nchi. Hayo yamesemwa na Afisa Mdhamini wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Ali Suleiman wakati akizungumza na Wajasiriamali huko ukumbi wa Chama cha Wandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar Mkanjuni Chake chake Pemba. Amesema iwapo biashara hizo zitakuwa na kiwango kinachostahiki kutawasaidia bidhaa zao kupata Soko la uhakikia. Amesema   sasa hivi Ulimwengu uko katika mabadiliko ya Kidijitali, hivyo ni vyema wajasiriamali waendane na mabadiliko hayo waweze kuzalisha bidhaa ambazo zitaweza kuwapatia tija. Aidha amesema Changamoto kubwa ya Wajasiriamali ni ukosefu wa Masoko ya kuuzia bidhaa zao, hivyo wakizalisha biashara zenye viwango watauza katika masoko ya Afrika Mashariki. Alifahamisha kuwa endapo wataweza kuzalisha biashara zenye viwango watapata wateja kwa wingi na kukuza uchumi wao na kuondokana na hali ngumu ya maisha.  

Umaskini ni moja ya chanzo za udhalilishaji.

Image
  UMASKINI uliokithiri   imebainika kuwa   ni moja ya   sababu inayopelekea   Watoto    kufanyiwa   Udhalilishaji. Hayo yamesemwa na mdau wa mtandao wa kupinga udhalilishaji kutoka Wilaya ya Mkoani, katika mkutano wa uwasilishaji wa ripoti za utekelezaji wa majukumu yao ya kutoa elimu   juu ya madhara ya udhalilishaji wa kijinsia kwa jamii uliofanyika ofisi ya TAMWA Pemba. Kwa upande wake Shaaban Juma Kassim Msaidizi wa sheria kutoka   shehia ya Mkanyageni, alifahamisha   kuwa udhalilishaji unafanyika zaidi kwa watoto   wanaokosa   malezi   ya   pamoja   ambao wazazi wao wameachana. Alisema   takribani   watoto   wengi ambao wazazi wao wameachana, wanakosa masomo na badala yake wanatumikishwa ili wapate mahitaji yao   hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya watoto. ‘’Wanawake wengi hususan wanaoishi vijijini ni maskini, hivyo hushindwa kuwalea watoto ipasavyo na kupelekea kudhalilishwa’’,alisema Shaaban. Nae Afisa Tathmini na ufuatiliaji wa chama cha Wandishi wa habari Wana

Rushwa muhali bado ni tatizo kukomesha vitendo vya Udhalilishaji.

Image
  Licha ya juhudi mbali mbali zinazochukuliwa na Serikali pamoja na Asasi za kiraia kuielimisha Jamii madhara ya Udhalilishaji wa kijinsia kwa Watoto  na jinsi ya kutoa ushahidi kwa kesi hizo lakini bado inaonekana matendo hayo  yanaendelea kujitokeza  kutokana na Muhali uliopo kwa Wanajamii. Hayo yamesema na wajumbe wa Mtandao wa  kupinga Udhalilishaji kutoka Wilaya ya Mkoani  katika kikao  cha uwasilishaji wa ripoti za utekelezaji wa majukumu yao ya kutoa Elimu  juu ya madhara ya Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Jamii huko ukumbi wa Chama cha Wandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar  [ Tamwma]  Mkanjuni Chake chake Pemba. Wanajamii hao. Wamesema Jamii inaonekana kuyafumbia macho na kuyafanyia suluhu Mitaani matendo ya udhalilishaji jambo ambalo linasababisha kuongezeka sikuhadi siku. Aidha wameeleza kuwa kuwepo  kwa umasikini uliokithiri imedaiwa kuwa ni moja ya sababu inayopelekea kuongezeka  kwa udhalilishaji kwa Watoto