Viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa mwanamke kushika nafasi za ungozi katika ngazi mbali mbali za kutunga Sheria. Akizungumza na viongozi wa dini ya kiislamu Kisiwani Pemba Afisa fatwa kutoka ofisi ya Mufti Sheikh Said Ahmad Muhammed katika mkutano wa uwasilishwaji wa ripoti ya miezi mitatu juu ya mwanamke kuwa kiongozi huko Tamwa Chake chake Pemba. Sheikh Said alisema Uislamu hauja mkataza mwanamke kua kiongozi ilihali tu afuate Sheria,Mila na Maadili yake . ‘’Dini haijamzuia mwanamke kuwa kiongozi bali afuate sheria na Madili ya dini yake’’ Alisema Sheikh Said. Hivyo alisema wakati umefika kwa viongozi wa dini mbali mbali kutoa elimu kwa jamii ili kuhakikisha mwanamke nayeye anashiriki katika nafasi mbali mbali za uongozi. Aidha Shikh Said amewataka wazazi na Walezi kutowabagua watoto Kijinsia katika kutoa fursa za kuwapatia Elimu. Wakichangia katika mkutano huo baadhi ya viongozi hao walisema kuwa ipo haja ya kutolewa