UTELEKEZWAJI WA WANAWAKE UNAVYOCHANGIA KUONGEZEKA KWA UDHALILISHAJI
NA FATMA HAMAD,PEMBA Utelekezwaji wa Wanawake na Watoto imedaiwa ni moja ya sababu inayo changia kutokea kwa vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa, kulawitiwa, kwa watoto. Hayo yamesemwa na hakimu wa Mahakama maalumu ya kupambana na Udhalilishaji iliyopo Wete, Muumin Ali Juma wakati akizungumza na Wananchi katika mkutano malumu wa kuwaelimisha Wananchi umuhimu wa kuripoti na kutoa ushahidi Mahakamani huko Chamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. Alisema wilaya ya Micheweni ni moja ya wilaya inayongoza kwa utelekezaji wa wanawake, katika mkoa wa Kaskazini Pemba jambo ambalo linachangia watoto kudhalilishwa. ,,Unamuacha mwanamke na watoto humpi huduma yoyote jee umetegemea nini, niwaulize wanaume wenzangu kesho mbele ya Mungu tutakwenda kujibu nini,aliuliza. Alisema mara nyingi kesi zinazofikishwa mahakamani za waliofanyiwa udhalilishaji ni watoto ambao wamekosa malezi ya pamoja kati ya Baba na Mama, hivyo aliwataka wananchi ha