Posts

Showing posts from March, 2024

WANDISHI WA HABARI WATAKA MABADILIKO KWENYE VIFUNGU VYA SHERIA AMBAVYO VINANYIMA UHURU WA HABARI

Image
    NA FATMA HAMAD,PEMBA                                                                 Wandishi wa habari wametakiwa kutumia taluma yao kwa kuvisemea vipengele vilivyomo kwenye sheria za habari ambavyo vimekuwa vikiwandamiza wandishi pamoja na vyombo vya habari katika utekelezaji wa kazi zao ili viweze kurekebishwa. Hayo yamesemwa na Shifaa Said Hassan kutoka baraza la Habari Tanzania [MCT] wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wandishi wa habari kuhusu masuala ya habari yaliofanyika ukumbi wa TAMWA Mkanjuni Chake chake Pemba. Alisema miongoni mwa vifungu ambavyo vimekuwa ni kikwazo kwa wandishi wa habari ni kifungu cha 4, na kifungu cha 27[1] vya sheria ya Usajili wa wakala wa habari Magazeti na vitabu No 5 ya mwaka 1988 iliyo rekebishwa na sheria no. 8 ya mwaka 1997. Aidha aliendelea kufahamisha kuwa vifungu vengine ambavyo vimekua ni kikwazo kwa wandishi wa habari pamoja na vyombo vya habari ni kifungu cha 6 [1] na 7[1] vya sheria ya Tume ya Utangazaji No. 7 ya mwaka