KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA PEMBA ZA TAKIWA KUWA WADILIFU WAKATI WA UKODISHWAJI WA MASHAMBA YA MIKARAFUU
NA LAILAT MSABAH PEMBA. Kamati za ulinzi na usalama katika mikoa miwili ya Pemba zimetakiwa kuwa makini katika kusimamia zoezi la ukodishwaji wa mashamba ya karafuu ya Serikali ili kuona misingi ya ukodishaji wa mashamba hayo inafuatwa na kuepusha upotevu wa mapato ya serikali. Akizungumza katika kikao na kamati iliyoonda kusimamia ha ukodishwaji wa mashamba hayo Mkuu wa Mkoa wa kaskazi Pemba Salama Mbarouk Khatibu amesema kamati hizo zinao wajibu mkubwa wa kuona mashamba ya karafuu yanakodishwa katika hali ya amani bila ya kuwepo na migogoro. ‘’Munadhamana kubwa kuhakikisha hakutokei migogoro yoyote wakati wa zoezi hilo la ukodishwaji mikarafuu’’ Alisema bi salama. Amewafahamisha kuwa endapo watasimamia zoezi hilo kwa uadilifu wa hali ya juu na kufuata taratibu zilizowekwa kutasaidia kuiongezea Serikali mapato yanayotokana na zao la karafuu. Mkuu wa wilaya ya Wete Mgeni Khatibu Yahya ameziomba kamati za ulinzi na usalama kufuatilia maeneo ambayo tayari uchumaji wa karafu