NUHU KOMBO NUHU AENDELEA KUSOTA RUMANDE
NA FATMA HAMAD-- PEMBA. Hatimae mahakama ya mkoa B Wete, imemrejesha tena rumande mtuhumiwa wa ulawiti Kombo Nuhu Kombo miaka 19 baada ya kubainika kuwa ni mtu mzima licha ya awali kupewa dhamana kama ni mtoto mahakamani hapo. Awali mtuhumiwa alipelekwa rumande mwanzoni mwa mwaka huu kwa tuhuma za ulawiti kwa kijana mwenye ulemavu wa akili ingawa upande wa utetezi ulidai na kuthibitisha kuwa mteja wao hakutendewa haki kupelekwa rumande kwa sababu ni mtoto. Wakati kesi yake ikiendelea miezi mitatu iliyopita na kuwasilishwa vielelezo mahakamani hapo na upande wa utetezi mahakamani iliridhia na kumpa dhamana mtuhumiwa huyo kama mtoto. Huku upande wa mashtaka ukiendelea kung’ang’ania kwamba mtuhumiwa ni mtu mzima, kisha uliwasilisha vielelezo kadhaa ikiwemo cheti cha kuzaliwa cha mtuhumiwa na mahakama kutengua uwamuzi wake wa awali juu ya umri wa mtuhumiwa. Mwendewsha mashtaka katika shauri hilo Juma Ali Juma alidai mahakamani hapo kuwa anaelewa kuwa mtuhumiwa Nuhu Ko