Posts

Showing posts from August, 2021

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA KWA AJALI BARABARANI

Image
 Watu wanne wameripotiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa kufuatia ajali  8  za  barabarani zilizotokea kwa mwezi  huu wa nane katika Mkoa wa Kusini Pemba. Akizungmza na wandishi wa habari huko ofisini kwake madungu kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Pemba ASP Richad Tadei Mchovu amesema kati ya watu hao wawili walifariki katika ajali ya piki piki na wawili ni katika ajali mbili tofauti za gari. Aidha amefahamisha kuwa ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa na uzembe wa madereva, kwani wamekuwa wakitembea mwendo kasi. ‘’Ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa na mwendo kasi walionayo madereva,’’ Alisema kamanda Mchovu. Hivyo amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za usalama wa barabarani wakati wanapoendesha vyombo vya moto,  jambo ambalo litaepusha ajali za kiholela.

WAZAZI WAHIMIZWA KUWAPATIA ELIMU WATOTO WENYE ULEMAVU

Image
  Wazazi na walezi wenye watoto walemavu wametakiwa kuwapeleka mashuleni pamoja   na madras ili waweze kupata elimu ambayo itawafaa katika maisha yao ya badae. Ushauri huo umetolewa na mmoja wa mzazi wa mtoto wenye ulemavu wa viungo   hapa kisiwani Pemba amesema watoto wenye ulemavu nawao wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine. Amesema wapo wazazi wamekua wakiwafungia ndani, watoto wao wenye ulemavu, jambo ambalo limekua likiwakosesha fursa mbali mbali ikiwemo elimu. ‘’Nawaomba wazazi wenzangu msiwafungie ndani watoto walemavu, kwani mkiwaeka ndani watakua wanadumaa na mnawatia maradhi, Alisema mama mwenye mtoto mlemavu. Amefihamisha kuwa watoto walemavu maranyingi hufanya   vizuri katika masomo yao ukilinganisha na wengine wasio na ulemavu. Akitoa ushuhuda amesema wakati mtoto wake   mlemavu hajapata kigari cha kuendea shule alikua hachangamki na alikua akiwaona wenzake wanakwenda shule akijitia chumbani na kulia. Hivyo kwa sasa amefanikiwa kupata kigari, anakwenda

MAKOSA 25 WIZI WA KARAFUU YARIPOTIWA POLISI KUSINI PEMBA MSIMU HUU.

Image
  Jumla ya matukio 25 ya wizi wa karafuu yameripotiwa katika Jeshi la   Polisi Mkoa wa Kusini Pemba tokea kuanza kwa msimu wa   mavuno ya karafuu mwaka huu. Akizungumza na wandishi wa habari huko ofisini kwake kamanda wa Polisi Mkoa   huo   Richad Tadei Mchovu amesema matukio hayo yalioripotiwa ni wizi wa karafuu mbichi. Aidha amesema katika matukio hayo pia wamefanikiwa kuwashikilia vijana 27 wanaojihusisha na uhalifu wa karafuu. Aidha amesema katika matukio hayo   makosa 12 tayari yamepelekwa   Mahakamani ambapo kijana mmoja ameshafungwa jela. Sambamba na hayo amewataka wananchi Kisiwani Pemba kuendelea na uchumaji wa zao la karafuu kwa Amani   bila kufanyiana vitendo vyovyote vya kihalifu. Amewataka wananchi kuuza karafuu   zao katika Shirika la ZSTC, ili wawezekuisadia Serikali mapato.  

UHABA WA WALIMU MJUMUISHO NI CHANGAMOTO KUBWA KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU MASKULINI

Image
Wazara   elimu na mafunzo ya amali Zanzibar imetakiwa kuwafundisha walimu wengi elimu mjumuisho   ili wawe na uwezo wa kuwasomesha wanafunzi wenye ulemavu maskulini. Hayo yamesemwa na mama wa Mtoto mwenye ulemavu wa viungo Siwawi Omar Said wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko nyumbani kwake   Kijichame wilaya ya Micheweni Pemba, amesema walimu wengi wanaofundisha maskulini hawana taaluma ya kufundishia wanafunzi wenye ulemavu. Amesema watoto wenye ulemavu wamekuwa wakipata shida, kwani hawaelewi wanachofundishwa, hivyo ni vyema wizara ya elimu kuwafundisha walimu lugha mbali mbali kulingana na mahitaji ya mlemavu mwenyewe. ‘’Ni vyema kuwepo na walimu wenye taluma ya kufndisha walemavu, kwani bila kufanyiwa hivyo wanakua hawaelewi lolote watakua wanakwenda wakicheza tu huko maskulini,’’ Alisema mama. Wadau wa elimu mjumuisho kisiwani Pemba wameiomba Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kupitia taasisi ya elimu kuangalia uwezekano wa kuingiza somo la watu we

WIZARA HABARI YATAKIWA KUINGIZA TIMU ZHA NETBAL KATIKA MASHINDANO YA MAWIZARA

    SALIM HAMAD,PEMBA MDAU wa Michezo Kisiwani Pemba Raya Mkoko Hassan ,Ameishauri Wizara ya Habari Vijana Sanaa na Michezo ambayo inaanda michuano ya mawizara  kuingiza  timu za Netbal katika mashindano ya Mawizara ili kuona  akina mama nao  wanapata nafasi za kuonesha Vipaji vyao.   Akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema Wizara ya habari inapaswa kuangalia suala hilo kwani nao akina mama  wana uwezo mkubwa wa kupambana kwenye mashindano kama hayo. Alisema kuwepo kwa mashindano hayo kwa upande wa Netbali itakuwa ni jambo zuri ambalo  litasadia kukuza uhusiano na Afya zao kutokana na kuwa michezo ni afya.   ‘’Tunaishauri Wizara husika iliyoandaa mashindano ya Mawizara kuangalia uwezekano wa kuingiza timu za Netbal ambazo zitaweza kuonesha uwezo na Vipaji  kwa akina mama ‘’alisema. Alisema kafuatia mashindano hayo yamewapa hamasa wanawake nao kuona wanakuwemo kwenye mashindano hayo kwa kila wizara kuwepo kwa timu moja ya wanawake ili waweze kufika mbali.   Hata

WIZARA YA AFYA YAHIDI KUBEBA UBINGWA YA WIZARA CUP

Image
SALIM HAMAD,PEMBA   BAADA ya kufanikiwa kutinga katika fainali ya Michuano ya Mawizara (Wizara Cup)  Nahodha wa timu ya Wizara ya Afya Abdul Karim Abdi Heri ameapa kuwa watabeba ubingwa katika michuano hiyo.   Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kufanikiwa kutinga kwenye hatua hiyo kwa kuichapa timu ya Shirika la Umeme ‘’Zeco’’  mabao 2-0 katika mchezo wa Nusu Fainali  uliopigwa Uwanja wa Gombani, Nahodha huyo alisema ushindi huo umewapa asilimia kubwa ya kufanya  vizuri kwenye Fainali ya mashindano hayo.   Alisema haikuwa kazi rahisi kuweza kuwafunga wapinzani wao kutokana na wao kutafuta nafasi ya kuwania kucheza fainali ya Mashindano hayo ili waweze kubeba ubigwa kwamara ya kwanza tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo.   Alisema katika mchezo huo  walipambana na kuonesha umahiri mkubwa kwa kushinda mchezo huo uliokuwa mgumu kwenye hatua hiyo iliyo kuwa inawaniwa na wapinzani wao. ‘’Sisi tumejipanga sana katika mashindano hayo licha kuwa ni magumu lakini tunaahidi washab

KIJANA OMAR ALI HAJI ATUPWA RUMANDE KWA KUTISHIA AMANI.

Image
  Mahakama ya Mkoa C Chake chake imemsokomeza rumande   kijana Omar Ali Haji   mwenye umri wa miaka 18   mkaazi wa junda miti kiwani   akidaiwa   kutishia amani,   baada ya kushindwa kutimiza masharti ya zamana aliyopewa na mahakama hiyo. Hakimu wa mahakama hiyo Rashid   M Magendo   amesema kijana huyo ataendlea   kusota rumande   hadi tarehe 30/ mwezi huu kwa ajili ya kusikilizwa,   huku akiwa na wadhamini   wake wawili [2] na shilling laki tatu [30000], kwa ajili ya kupewa dhamana yake. Mtuhumiwa   huyo wakati yupo   kizimbani na kusubiri asomewe shitaka lake mwendesha mashtaka   wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP Mohd   Said Mohd amesema sena pingamizi nimekubaliana na uawamuzi huo. Imedaiwa kuwa siku ya tarehe 23/ 7/ mwaka huu majira ya sa moja   na nusu asubuhi   huko Junda miti   Kiwani wilaya ya Mkoani Pemba ulimshambulia kwa hatari Khamis Juma Ali kwa kumkata na Panga katika sehemu zake za mkononi na kusababisha kupata maumivu makali katika sehemu hizo

WANDISHI WA HABARI WAHAMASISHENI WANAUME KUPIMA VVU

Image
Wandishi wa hababari wametakiwa kuandika habari za Afya ya jamii ambazo zitatoa hamasa kwa Wanaume ili waweze kujitokeza Hospitali kupima VVU. Hayo yamesemwa na mkurugenzi wa tume ya ukimwi Zanzibar   [ZAC] Ahmed Mohd wakati akizungumza na wandishi wa habari huko Gombani chake, amesema wandishi wana mchango mkubwa juu ya kuwaelimisha wanaume kupima afya zao jambo ambalo litaepusha ongezeko la mambukizi mapya ya virusi vya ukimwi Nchini. Amesema imebainika kuwa idadi ya wanaume wanaojitokeza   vituoni mwa afya kupima VVU ni ndogo ukilinganisha na wanawake. ‘’Wanaume bado hawataki kupima afya zao, wengi ni wanawake ndio wanaozitumia huduma hizo,’’Amesema dk Ahmed. Amesema   wanaume wengi wanaogopa kupima   vvu kutokana   na kutokuwepo kwa usiri kwa baadhi ya madaktari wanaotoa huduma hizo, jambo ambalo linachangia   kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa mambukizi mapya ya virusi vya ukimwi. Amesema wanaume wengi kipimo chao kikubwa ni wake zao, kwani wanahisi wakishakwenda kupima na

WANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWAPA ELIMU JAMII JUU YA USULUHISHAJI WA MIGOGORO

Image
  Wandishi wa habari wametakiwa kuwaelimisha jamii kwa kuandika habari za utatuzi wa migogoro kama ya Siasa, Ndoa ili waweze kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima. Akizungumza katika mkutano juu ya namna ya utatuzi wa migogoro katika Jamii Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka kituo cha huduma za sheria Zanzibar Khamis Haroun Hamad huko gombani Chake chake Pemba. Amesema   wandishi wana nafasi kubwa katika jamii hivyo ni wajibu kutumia kalamu zao kwa kuielimisha jamii kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima jambo ambalo litapelekea kuvunjika kwa Amani. Amesema suala la kulinda amani si la mtu peke yake bali kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa achukue tahadhari juu ya kulinda haki za mwenzake. Mapema mratibu wa mradi wa Jenga amani yetu   kutoka kituo cha huduma za sheria Zanzibar Jamila Masoud amesema wakati umefika kwa wandishi wa habari kujikita zaid Vijijini katika kazi zao jambo ambalo litawasaidia kuibua migogoro ambayo inajitokeza na kuweza kuzitolea suluhu. Nao baadhi y

TASISI ZA KIHABARI ZATAKIWA KUWEKA SERA ZA UDHALILISHAJI

  NA FATMA HAMAD FAKI. Mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania [TAMWA] Joic   Shebe   amesema kuweko na mfumo maalum ambao utawasaidia wandishi wa habari kuripoti malalamiko yao wakati wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono katika tasisi zao. Mwenye kiti huyo ameyasemahayo katika mdahalo kuhusu unyanyasaji wa kingono katika tathnia ya habar   kwa wandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya mtandao amesema bado wandishi wa habari wanawake wanakumbana na unyanyasaji wa kingono wakati wanapokua katika harakati zao za kazi. Amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa unaonesha kuwa kila   penye watu wawili mmoja amefanyiwa unyanyasaji, hivyi ni vyema kwa vyombo vya habari   vitunge sera   na kuhakikisha zinafuatwa kwa mujibu wa sheria ili kutoa adhabu kali kwa wale watakao jihusisha na vitendo hivyo. Akiwasilisha mada ya sera ya jinsia katika vyombo vya habari   Nevil Meena   amesema wandishi wa habari ndio mwanga kwa jamii, hivyo wasikubali kufanyiwa unyanyasaji wa

TASISI ZA KIHABARI ZATAKIWA KUWEKA SERA ZA UDHALILISHAJI.

  NA FATMA HAMAD FAKI. Mwenyekiti wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania [TAMWA] Joic   Shebe   amesema kuweko na mfumo maalum  katika vyombo vya habari ambao utawasaidia wandishi wa habari kuripoti malalamiko yao wakati wanapofanyiwa unyanyasaji wa kingono katika tasisi zao. Mwenye kiti huyo ameyasemahayo katika mdahalo kuhusu unyanyasaji wa kingono katika tathnia ya habar   kwa wandishi wa habari uliofanyika kwa njia ya mtandao amesema bado wandishi wa habari wanawake wanakumbana na unyanyasaji wa kingono wakati wanapokua katika harakati zao za kazi. Amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa unaonesha kuwa kila   penye watu wawili mmoja amefanyiwa unyanyasaji, hivyi ni vyema kwa vyombo vya habari   vitunge sera   na kuhakikisha zinafuatwa kwa mujibu wa sheria ili kutoa adhabu kali kwa wale watakao jihusisha na vitendo hivyo. Akiwasilisha mada ya sera ya jinsia katika vyombo vya habari   Nevil Meena   amesema wandishi wa habari ndio mwanga kwa jamii, hivyo wasikubali

CHANJO INAYOENDELEA KUTOLEWA KISIWANI PEMBA NI KWA AJILI YA KIPINDU PINDU NA SIO KWA AJILI YA KORONA WANANCHI WATOLEWA HOFU

Image
NA FATMA HAMAD FAKI PEMBA. Mratibu wa huduma ya chanjo   kisiwani Pemba Bakar Hamad Bakar  amewatoa hofu Wananchi kuwa  chanjo inayoendelea kutolewa kisiwani hapa     ni kwa ajili ya kinga dhidi ya kipindu pindu na  sio ya kinga dhidi ya  Corona, kama wananchi wanavosema.  Bakar ameyasema hayo wakati akizungumza    na  waandishi wa habari kufuatia  kuzuka  kwa zana juu ya chanjo ya kipindu pindu inayotolewa. Alisema, kwa sasa wizara ya Afya inaendelea na awamu ya pili ya chanjo hiyo kwa njia ya matone, kwa wananchi waliopata awamu  ya kwanza. Alieleza kuwa, sio sahihi kuwa chanjo hiyo ni ya Corona, kama wanavosema  kwani chanzo ya Corona haitolewi kwa njia matone. “Niwatowe wasi wasi wananchi kuwa, hii inayoendelea kwa sasa sio chanjo kwa ajili ya Corona, bali ni kwa ajili ya kipindupindu, hivyo wajitokeze kumaliza dozi awamu ya pili,’’alieleza. Aidha Mratibu huyo alisema, bado chanjo ya Corona haijawasili kisiwani Pemba, na hivyo ikiwasili wananchi wote watapewa taarifa . Alifafanua d

.AJIRA BADO NI KIKWAZO KWA WATU WENYE ULEMAVU

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA. JAMII ya watu wenye ulemavu kisiwani Pemba wanalalamikia upatikanaji mdogo wa furusa ya ushirikishwaji katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo katika jamii ikiwemo suala la ajira. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Chake chake   mwenyekiti wa jumuia   ya watu wasiona ZANAP   Suleiman Mansour amesema watu wa jamii hiyo wamekua wakiwekwa nyuma     katika fursa za kimaendeleo wakati zinapotokezea katika jamii au za kiserikali ikiwemo suala zima la nafasi za   ajira. ‘’ ushiriki wa watu wenye ulemavu katika sekta ya Ajira bado ni wa kusuwa suwa sana, Alidai   mwenyekiti”. Amesema ni vyema kwa Serikali kuweka mpango mkakati wa kuhakikisha kuna kuwepo na idadi stahiki ya watu wenye ulemavu katika nafasi   mbali mbali za uajiri.   Mratibu wa idara ya watu wenye ulemavu Pemba Mashavu Juma Mabrouk amesema sheria ya watu wenye ulemavu imesema walemavu wanahaki sawa ya kupata ajira, hivyo   idara yake imekua ikifanya kila jitihada ili kuona wat

WANDISHI WATAKIWA KURIPOTI MATATIZO YAO MCT WAKATI YANAPOWATOKEZEA

Image
  WAANDISHI wa habari nchini, wametakiwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania [MCT] kutoa malalamiko yao wakati wanapopata matatizo katika majukumu yao ya kazi. Hayo yamesemwa na Afisa ufuatiliaji na tathmini wa MCT   Paul Mallimbo   wakati akizungumza na wandishi wa habari huko Zanzibar, ambapo amesema Baraza kwa kuwajali wandishi wa habari, limeweka utaratibu wa kupokea kero zinazowakumba ikiwemo kupigwa, kutukanwa, kunyimwa taarifa ili kuweza kutoa msaada kwao. Amesema imeonekana bado wandishi hawajakuwa na mwamko wa kuripoti matatizo yao, wakati yanapowatokezea na jambo ambalo linawanyima fursa yao ya kufanya kazi zao kwa umakini. Kwa upande mwengine ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kutoa mashirikiano ya hali ya juu wandishi wa habari, jambo ambalo itawafanya waweze kuandika na kuripoti habari zenye ukweli na zenye kuleta mabadiliko mazuri katika Jamii. Mapema Mtendaji wa Baraza la habari Tanzania [ MCT] ofisi ya Zanzibar Shifaa Said Hassan, amewasihi wandishi w

AFUNGWA KWA KUBAKA

Image
    Kushindwa kudhibiti matamanio yake kumempelekea   Kijana Thani Khamis Mohd 22 mkaazi wa Kinyasini Mkoani Pemba kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka 14, pamoja na fidia ya shiling milioni mbili   (2,000,000)/. Hakimu wa mahakama ya mkoa A Chake chake Abdul Razak Abdul kadir amesema hukumu hiyo imekuja baada ya mahakama yake kujiridhisha kutokana na ushahidi uliotolewa na mashahidi. Hivyo mahakama imeamua kumtia hatiani mtuhumiwa huyo, na endapo atashindwa kulipa fidia atatumikia tena kifungo cha miezi 6. ‘’Mahakama yangu imeridhika na ushahidi uliotolewa ndipo ikatoa hukumu na endapo atashindwa kulipa fidiya atatumikia tena kifungo cha miezi 6,’’ alisema hakimu. Mwendesha   mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Seif Mohamed Khamis amekubaliana na hukumu hiyo, kwani itakua ni fundisho kwa wabakaji. Aidha amewataka wananchi kushirikiana na mahakama kutoa ushahidi   ili kuona kesi za udhalilishaji zinapata hatia jambo ambalo litapunguza vitendo h