.AJIRA BADO NI KIKWAZO KWA WATU WENYE ULEMAVU




 

NA FATMA HAMAD PEMBA.

JAMII ya watu wenye ulemavu kisiwani Pemba wanalalamikia upatikanaji mdogo wa furusa ya ushirikishwaji katika mambo mbali mbali ya kimaendeleo katika jamii ikiwemo suala la ajira.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake Chake chake  mwenyekiti wa jumuia  ya watu wasiona ZANAP  Suleiman Mansour amesema watu wa jamii hiyo wamekua wakiwekwa nyuma   katika fursa za kimaendeleo wakati zinapotokezea katika jamii au za kiserikali ikiwemo suala zima la nafasi za  ajira.

‘’ ushiriki wa watu wenye ulemavu katika sekta ya Ajira bado ni wa kusuwa suwa sana, Alidai  mwenyekiti”.

Amesema ni vyema kwa Serikali kuweka mpango mkakati wa kuhakikisha kuna kuwepo na idadi stahiki ya watu wenye ulemavu katika nafasi  mbali mbali za uajiri.



  Mratibu wa idara ya watu wenye ulemavu Pemba Mashavu Juma Mabrouk amesema sheria ya watu wenye ulemavu imesema walemavu wanahaki sawa ya kupata ajira, hivyo  idara yake imekua ikifanya kila jitihada ili kuona watu wenye ulemavu na wao wanapata fursa sawa wakati zinapotokezea.

 Hivyo amewataka watu wenye ulemavu wasikate tamaa kutokana na hali walizo nazo bali wajiendeleze kielimu jambo amblo litawasaidia kukidhi vigezo vinavo stahiki katika mfumo mzima wa ajira.



Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.