JAMII YAHIMIZWA KUTUNZA USAFFI MAZINGIRA
NA SAID ABRAHMAN PEMBA. WANAJAMII wametakiwa kutunza mazingira yao na kuhifadhi maji taka ( maji machafu) ili kuepusha maradhi ya mripuko yanayoweza kutokezea katika maeneo yao. Hayo yalielezwa na Bwana afya kutoka Baraza la Mji Wete Salim Mbarouk Rashid wakati alipokuwa akizungumza na Mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Wete. Alieleza kuwa kumekuwepo na utiririkaji Mkubwa wa maji taka (machafu) katika majumba jambo ambalo ni tatizo kubwa Kimazingira na hivyo kufanya mazingira kuwa katika hatari na kuwa Kero katika jamii. "Kutokana na Hali ambayo ipo katika jamii,suala la kutiririka Kwa maji taka linahatarisha afya Kwa wananchi na hivyo kupelekea kuibuka Kwa maradhi mbali mbali ya miripuko ikiwemo matumbo na kipindupindu," alieleza Salum. Aidha Salim alifahamisha kuwa ikiwa Baraza la Mji Wete ndio wasimamizi wakuu wa Usafi katika Mji wamekuwa na mikakati mbali mbali ili kuona hali hiyo inapungua au kuondoka kabisa katika jamii. "Mikakati