Watendaji wa wizara ya maji kisiwani, Pemba wamelalamikia kunyimwa haki zao
Watendaji wa wizara ya maji kisiwani, Pemba wamelalamikia juu ya ukosefu wa haki na fursa za kielimu ambazo zimekua zikipatikana kupitia wizara hio kwa muda mrefu sasa. Malalamiko hayo wameyatoa mbele ya waziri wa wizara ya maji na nishati Zanzibar Sleimani Masoud Makame,wakati alipokutana na watendaji wa wizara hio kisiwani Pemba ambapo watendaji hao wamedai kua wamekua wakikoseshwa fursa mbalimbali kutoka wizara hiyo ikiwemo fursa ya mafumzo. ‘’Mheshimiwa Waziri Mkurugenzi wetu mtu aliekua hana elimu ndio anaempa kipao mbele na maranyingi huwateuwa nafasi kubwa wale waliokua hawana elimu’’Walisema wafanyakazi wa wizara hiyo. Baada ya kupokea malalamiko hayo waziri wa wizara hio amemuagiza mkurugenzi wa mamlaka ya maji Pemba Omari Mshindo Bakari, kushughulikia upatikanaji wa stahiki za wafanyakazi hao. ‘’Mkurugenzi naomba kuanzia sasa kila mmoja hakikisha anapata haki yake, sitaki kuletewa tena malalamiko ya mtu kakosa haki yake’’Alisema Waziri. Aidha waziri huyo amew