Posts

WANAHABARI, WADAU WAOMBA VIFUNGU VINAVYOMINYA UHURU WA HABARI VIREKEBISHWE

Image
                                                NA FATMA HAMAD,PEMBA KILA baada ya miaka 10 sheria huwa zinahitaji kubadilishwa ili kuondosha mapungufu ya vifungu ambavyo vitakua haviendani na utekelezaji wa sheria hiyo.   Ijapo kuwa wakati mwengine sio lazima kusubiriwe hadi itimie miaka 10 ndio   iweze kufanyiwa marekebisho. Na hii itasaidia kuweka sawa vifungu vyenye mapungufu ili viweze kuendana na muda na mazingira ya sasa. Lakini tukiangalia sheria ya Usajili wa Uwakala wa habari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanywa marekebisho na Sheria Namba 8 ya mwaka 1997, haiendani na mazingira ya sasa kwani ni  kongwe hivyo inahitajika ifanyiwe marekebisho. Takriban ni miaka 26 tangu Sheria hiyo kufanyiwa marekebisho ingawa bado baadhi ya vifungu vyake vina mapungufu ambavyo vinaminya uhuru habari. Miongoni mwa vifungu hivyo ni kifungu cha 30 kinachompa   mamlaka makubwa   Waziri kiasi ambacho kinaminya uhuru wa habari pamoja na kifungu cha 27[1], 27[2].   A

DK MWINYI AWAFURAHISHA WANANCHI PEMBA

Image
      *RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza ujenzi wa miundombinu imara kwa Sekta za Maendeleo nchini.*  Dk. Mwinyi ameeleza hayo uwanja wa Jamuhuri wa Skuli ya Sekondari Utaani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, alipofungua skuli ya Sekondari ya wanawake ya Ghorofa tatu iliyojengwa upya na serikali baada ya kupata ajali ya kuunga moto na kuteketeza kila kitu Mwezi Machi mwaka 2022.  Alisema, ujenzi wa skuli hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya serikali iliyoitoa baada ya tukio la moto lililoteketeza skuli ya awali iliyokuwa na madasa 11 na kuahidi kujenga skuli bora zaidi ambayo kwasasa ina madarasa 41.  Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameahidi kujenga dahalia kubwa ya kisasa itakayoendana na hadhi ya skuli hiyo.  Katika kuboresha haiba njema ya mandhari mpya ya eneo la skuli hiyo, Rais Dk. Mwinyi ameiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kusimamia ujenzi uliobakia wa ukumbi wa mi

WALIMU WATAKIWA KUVIANDAA NA KUVITUNZA VIPAJI VYA MICHEZO MASKULINI ILI VIWEZE KUFANYA VIZURI KATIKA MASHINDANO

Image
                      NA FATMA HAMAD,PEMBA Timu ya Netball ya Wasichana imejipanga kufanya vizuri katika michuano ya elimu bila malipo inayotarajia kuanza hivi karibuni.   Mashindano hayo hufanyika kila mwaka na kushirikisha Skuli za Msingi na Sekondari zilizopo Unguja na Pemba, kwa michezo tofauti ikiwemo Natball.  Akizungumza na Pemba ya leo Blog   Fatma Abdalla alisema kwa vile mwaka jana hawakufanya vizuri, mwaka huu wamedhamiria kutwaa ubingwa kwenye mashindano hayo.  Alisema Kwa sasa wanafanya maandalizi kwa kufanya mazoezi ili waweze kufikia ndoto zao walizojiwekea katika timu yao.  Alisema unapofanya maandalizi mapema mara nyingi inakuwa unajiweka kwenye nafasi nzuri .  "Unajua sisi lengo letu kufanya maandalizi mapema tunataka kufanya mazuri ambayo yataisaidia timu hiyo "alisema.     Hivyo aliwataka wanatimu hao wasivunjike moyo bali waendelee kubambana kihali na mali ili kuhakikisha mwaka huu wanashika nafasi ya mwanzo.            

WANAWAKE WATAKIWA KUWA NA UTHUBUTU ILI WAWEZE KUSHIKA NAFASI ZA UONGOZI

Image
                          NA NIHIFADHI ISSA,UNGUJA WANAWAKE WAMETAKIWA KUTOKUVUNJIKA MOYO PINDI WAKIKOSA NAFASI WALIYOGOMBANIA    BALI WAZIDI KUONESHA ARI   UTHUBUTU, KUJIAMINI NA KUSOMA MAMBO MBALIMBALI ILI KUFIKIA LENGO LA KUWAPAMBANIA WENGINE WITO HUO UMETOLEWA NA NAIBU SPIKA ZANZIBAR    LAKINI   PIA NI MWAKILISHI KUPITIA VITI MAALUM UWT MKOA WA MJINI      MGENI HASSAN JUMA WAKATI AKIZUNGUMZA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI HUKO NYUMBANI KWAKE TUNGUU MKOA WA KUSINI UNGUJA MH MGENI AMBAE NI NAIBU SPIKA WA KWANZA MWANAMKE WA BARAZA LA WAWAKILISHI HAPA ZANZIBAR AMESEMA HAKUWA NA NDOTO ZA KUWA KIONGOZI KWANI KITAALUMA ALIKUWA MWALIMU LAKINI CHANGAMOTO ZA WANAWAKE NA WATOTO   ZILIMSUKUMA KUINGIA KWENYE SIASA MWAKA 2010 NA KUWA KIONGOZI   ILI KUWA MTETEZI WAO KATIKA NGAZI ZA MAAMUZI ALISEMA KUTOKANA NA ULIMWENGU KUBADILIKA WANAWAKE WANATAKIWA KUJIKITA KWENYE ELIMU   AMBAYO ITAMSAIDIA KUJENGA HOJA NA KUJIAMINI KATIKA KUFIKIA NDOTO ZA KUWA KIONGOZI ALI SULEIMAN SHIHATA MWAKILISHI