UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI
NA FATMA HAMAD, PEMBA
WANAWAKE
wanne pekee wa shehia ya Mchanga mdogo ambao ni wanaufaika wa mfradi wa Zanzibar Women Leadership in Adaptation (ZAN
ADAPT) wako mbioni kuuwaga umaskini wa kipato.
Matumaini
yao, yanakuja kufuatia wote kwa pamoja kumiliki miti ya biashara na chakula
3,379 ambayo yanaweza kuwaingizia zaidi ya shilingi Milioni 10.7.
Wanamiliki miembe 22 , wakiamini kama itaaza
yote watajivunia wastani wa embe 1,1000 na pindi wakiyauza kwa bei ya juma ya
shilingi 500, watajipatia jumla ya shilingi ya shilingi milioni 5,500,000.
Miti
mingine wanayomiliki ni Miparachichi 9, ambapo kwa mujibu wa Mwanafunzi
anaefanya Digrii ya kilimo katika Chuo
cha Kilimo na Technology cha Mwalimu Nyerere (MNUAT) kilichopo Musoma Tanzania
bara Makame Jafar Juma, anasema kila mmoja, unauwezo wa kuzaa maparachichi kati ya
200 hadi 250, kutegemeana na mazingira.
Anafahamisha
kuwa miche hiyo iko ya aina mbili ikiwa ni pamoja na ya muda mfupi na ya muda
mrefu, ambapo hata uzaaji wake inategemeana na mazingira ya ardhi yenyewe na
ushughulikiaji wenyewe.
Sasa
wanawake hawa, wenyewe huwenda wakajipatia matunda hayo 2,250 ambapo kwa bei ya
jumla ya sokoni ni shilingi 700, na kujipatia shilingi milioni 1.5
Fatma Hamad Bakar, alimueleza mwandishi wa makala hii, kuwa katika kilimo
chao msitu, kwa sasa wanamiliki migomba 412, ya mkono mmoja.
Kumbe
wanawake hawa kupitia mradi huu wa mabadiliko tabia nchi, wanategemea kujipatia
wastani wa shilingi Milioni 3,296,000 ikiwa wataiuza ndizi moja kwa bei ya jumla ya shilingi 8000.
Mwengine ni Zaitun Hassan Ali,
anasema yeye peke yake anayo minanasi 497, anategemea kupata wastani wa
shilingi Milioni 8.4 baada ya kuuza kila nanasi moja kwa shilingi 1700.
‘’Mimi peke yangu nategemea kujichukulia
wastani wa shilling Milioni 8.4 kupitia kilimo cha minanasi, na tena kwa msimu
mmoja tu,’’anasema.
Pia
wamawake hao wanaeleza kwamba baada ya mafunzo ya kilimo msitu walioyapata
kutoka Tamwa waliamua kupanda
Midalasini, ambapo wanayo 434, katika mashamba yao.
‘’Ndugu muandishi baada ya miaka mitatu
Mchangamdogo kila kona utakayopita utasikia harufu ya Pilau, kwani midalasini
yetu hiyi itakua imeshapea (imeshakomaa).
Wanasema
kwa msimu wa kwanza wanamatumaini ya kuzitia mkononi wastani wa Shilingi
Miliono 45,570,000, kupitia kilimo cha Midalasini ndani ya msimu mmoja tu.
LAKINI JEE HOFU YAO WANAWAKE HAO NI IPI JUU YA SHUGHULI ZAO HIZO
Wakulima
hao wanawake wanaeleza kwamba wanahofu ya kuja kuzikosa pesa hizo katika misimu
mwingine kwani, wanahofu ya kupokonywa
mashamba ambayo wanafanyia shughuli zao hizo za kilimo, kwa vile si za kwao bali
ni za waume zao.
Fatma
Hamad Bakar ni mmoja wa wanawake hao wakulima, anasema shamba analotumia kufanya shughuli hizo za
kilimo msitu sio la kwake, bali ni
la mama wa marehemu mume wake.
‘’Sina
shamba langu mwenyewe, nalima kwenye shamba la mamayake marehemu mume wangu,
mimi sijarisishwa ardhi katika familia yangu, kwani hakuna utaratibu wa
kurithishana’’anasema.
Mwengine
ni Zaitun Hassan Ali anasema shughuli
zake za kilimo msitu anazifanya katika
shamba la mume wake, yeye hana ardhi yake mwenyewe.
Anasema
yeye, familiani kwao wanayomashamba, ingwa licha ya kua wazazi wao
wameshaondoka lakini yanabakia katika mikono ya ndugu zao.
‘’Hata
ukijaribu kudai utaambiwa wewe shamba la kazi gani wakati umeolewa mbali, sasa
utalihudumia vipi,’’anaeleza.
Mwanamke
mwengine ni Maryam Ali Juma (sio jina lake halisi) kutoka shehia jirani ya
Mchangamdogo, anasema yeye alirithi shamba baada ya kufa wazazi wake,
ingawa kaka zake walishampokonya,
wanalitumia wao.
‘’Baada
ya kufariki wazazi wetu tulirithi, ingawa kakazangu wameshanipokonya, na sasa
nalima kwenye shamba la mume wangu,’’anasema.
Asha
Khamis wa Mchangamdogo anasema yeye
shamba analotumia kulima kilimo hicho ni la kwake mwenyewe.
Anasema
aliamua kununua shamba lake mwenyewe ili afanye shughuli za kilimo ambazo
zitaweza kumuingizia kipato, na hakuweza kutegemea shamba la ukoo.
Anasema hakutaka kuja kusumbuana na familia yake kwa
suala urithi, bali alidunduliza pesa zake hadi akafanikiwa kununua shamba lake
mwenyewe.
‘’Nilianza kudunduliza pesa katika biashara
zangu za kachori, mandazi na malai, hadi
nikatimiza nikanunua, na sasa nalima
shambani kwangu mwenyewe,’’anasema.
Hamad Haji Suleiman ni mume kati ya miongoni mwa mama hao anasema amamua kutoa shamba lake kumpa mke wake afanyeshughuli hizo za kilimo, kwa vile hana shamba lake mwenyewe kwani nyumbani kwao hajapewa, na wala hana uwezo wa kununua shamba.
''Kwa vile shughuli hizo anazozifanya mkewangu za kilimo msitu ni jambo muhimu katika maisha yetu nimeamua kumpa shmba langu mimi mwenyewe ambalo nimelipata katika familia yangu kumpa alime tupate mazao ya chakula, pesa na huku tukinga na athari za mabadiliko ya tabianchi,''anasema.
Anasema ni kweli wengi wa wakulima hao hawanamashamba yao wenyewe, kwani hawana uwezo wa kununua, na familia nyingi wanapofariki wazazi wao wanaona mwanamke kurithi ardhi sio jambo la muhimu kwake, wanahisi hawawezi kulihudumia ahata akipewa, kwa vile wao ni watu wa kuolewa na kuhamia sehemu nyengine.
JAMII
Maimuna
Ali Khamis (sio jina lake halisi) mwananchi kutoka Micheweni anasema familia
nyingi zinapofariki wazazi wao hawana utaratibu wa kurithi kama kuna mali
zilizoachwa zaidi hwanufaisha wanaumetu, hali inayowafanya wanawake kuhangaika kwa
kukosa rasilimali shamba za kuzalisha mazao
na kujipatia kipato.
Omar
Khamis Kombo (sio jina halisi) kutoka
Maziwangombe micheweni anasema sababu kubwa inayopelekea wanamke siku zote
kukosa ardhi zao wenyewe ni
kutokuonekana, kama hawana haki ya kurithi na kumiliki.
WANAHARAKATI
Sada Juma Segeja mtetezi wa masuala ya
wanawake kutoka Jumuia ya Uhifadhi wa misitu Pemba CFP, anasema moja ya
changamoto inayowakabili katika mradi
wao wa uhifadhi mazingira ni baadhi ya wanawake kukosa Ardhi zao wenyewe.
‘’Hofu
yetu ni pale ambapo mwanamke ataachika, jee zile nguvu zake ashazozipoteza kwa
kupanda Misitu itakuaje, wakati shamba ni la mume walieachana.
Anasema kwa sasa wamekua wakiwapatia elimu ya
ujasiriamali wafanye biashara wapate pesa wanunue mashamba yao wenyewe, pamoja
na kupata hatimiliki kwa walio na shamba
zao wenyewe.
Mkuu
wa kitengo cha mawasiliano kutoka Chama
cha Wandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar, Sofia Ngalapi anasema wamekua
wakitoa elimu mara kwa mara kwa jamii, ili ifahamu umuhimu wa mirathi, na kuona
mwanamke ana uwezo wa kumiliki mali za marehemu wazazi wake ikiwemo ya ardhi.
MWANASHERIA
Naibu
Mrajisi kutoka Kamisheni ya ardhi Pemba Asha
Suleiman Said anasema kwa mujibu wa Sheria ya ardhi namba 12 ya mwaka
1992 inaeleza kuwa ardhi ya Zanzibar ni mali ya umma, hivyo kila mwananchi
anahaki ya kutumia ardhi.
Anasema
katika Kifungu cha saba cha Sheria hiyo
kinaeleza kwamba haki ya kutumia
ardhi ya Zanziba ni kwa wazanzibari tu.
Akitaja
moja ya njia ambayo mtu anaweza kupata ardhi na kutumia ni kurithi baada ya
kufariki kwa wazazi wake.
‘’Sheria
ya ardhi inalitambua suala la mirathi, hivyo
anapofariki mtu wale warathi wafike Kamisheni ya Wakfu na
maliamana,kupata taratibu za mirathi na kupa hatimiliki,’’anaeleza.
VIONGOZI
WA DINI
Asya
Amour Abrahman Amirati kutoka Jumuiya ya
wanawake wa kiislamu Pemba (JUMA WA KIPE) anasema kwa mujibu wa Sheria ya Dini ya Uislamu mwanamke
anahaki ya kumiliki Ardhi.
‘’Mwanamke anahaki ya kumiliki ardhi na akaweza kuitumia kwa shughuli za kilimo,
na akajipatia kipato kutokana na Shamba lake, isipokua kuna mipaka yake katika
suala la mirathi tu,’’anafafanua.
Anasema
mwanamke anahaki ya kufanya shughuli zozote za kimaendeleo na kujipatia kipato
ambacho kinakubalika katika
uislamu.
Kiongozi
wa Kanisa Katoliki lililopo Mkungu Malofa Chake chake mkoa wa Kusini Pemba Robert Miguwa Ndalami,
anasema mwanamke anahaki ya kumiliki
ardhi kama mwanamme, kwani hata dini yao haijamkataza asimiliki ardhi.
MIKATABA
Mkataba
wa Umoja wa Mataifa CEDAW wa mwaka 1986, unapiga marufuku ubaguzi wa kijinsia
katika umiliki wa mali.
Itifaki
ya Maputo (kifungu cha 21) inahakikisha wanawake wanapata urithi bila
kubaguliwa na tamaduni.
Mkurugenzi
wa Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania Tamwa Zanzibar Mzuri Issa Ali
anasema ijapokua Sheria zinasema kila mwanamke anahaki ya kumiliki ardhi,
ingawa bado kunaurasimu mkubwa juu ya jambo hilo
Kwa
mujibu wa Utafiti alioufanya Mkurugenzi
huyo, wa mwaka 2025, ulionesha
kuwa mitazamo ya jamii na vyombo vya habari vina nafasi kubwa katika kuendeleza
au kupunguza mitazamo hiyo potofu.
Takwimu
kutoka Ofisi ya Mtakwimu mku wa Serikali za mwaka 2014,/15, na 2019/20
zinaonesha kuwa ni asilimia 5.5 ya wanawake waliokua wanamiliki ardhi
ikilinganishwa na wanaume ambao ni asilimia 12,
hivyo inaonekana kuna pengo kubwa la kijinsia kumiliki rasilimali
muhimu.
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha
12 (a) kinaeleza kuwa watu wote ni sawa mbele ya Sheria, na wanayohaki, bila
ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya Sheria.
Makadirio ya
Bajeti kwa mwaka wa
Fedha 2023/2024 ya Wizara
ya Ardhi na
Maendeleo ya Makaazi,
Kuendelea kutoa elimu
kwa jamii kuepuka
kujiingiza kwenye migogoro
ya ardhi kwa kufuata
Sheria za ardhi.
Ripoti
ya Banki ya Dunia inaeleza kushindwa kuchukuliwa hatua za mabadiliko ya tabianchi,
kunaweza kupunguza ukuaji wa uchumi
Tanzania kwa asilimia nne ifikapo mwaka 2050.
ATHARI
YAKE
Endapo
wanawake watakosa Ardhi na kufanyashughuli za kuzalisha, daima wataishi katika
hali ya unyonge na pia zikitokezea athari za mabadiliko tabianchi zitawakumba
kwa haraka,’’wakulima wenyewe wanaeleza.
NINI
KIFANYIKE
Afisa
mawasiliano kutoka TAMWA Zanzibar Sophia Ngalapi anasema ipohaja kwa wanawake
kuamka na kuhakikisha wanafanya biashara japo ndogondogo, ili wanunue
mashamba yao wenyewe, na sio kutegemea za mirathi tu.
Comments
Post a Comment