Kiungoni walia na huduma ya Maji NA FATMA HAMAD, PEMBA WANACHI WA SHEHIA ya Kiuongoni wilaya ya Wete Kaskazini Pemba wamelalamikia juu ya kadhiya inayowakabili, ya ukosefu wa huduma za Maji safi na salama kijijini mwao. Wananchi hao walisema tokea ulipoanza ujenzi wa barabara suala la Maji ya Zawa vijijini mwao imekua ni kama ndoto, jambo linalopelekea usumbufu wa kutafuta huduma hiyo maeneo ya mbali. Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao, kiungoni mwananchi Zainab Abdallah Hassan na Ngindo Kombo Faki walisema wanategemea huduma ya maji kupitia Kisima cha Msikitini, ambapo kupandishwa kwake kwenye Tenki ni nadra, kwani hadi wananchi walipie pesa ndio yapandiswhe. ‘’ Hayo maji tunayotegemea hapo msikitini hayapatikani kama wananchi hawajachanga pesa, hivyo kupatikana kwake ni shida,’ walisema. Walisema kuwa tatizo hilo limeshakua kubwa na linahitaji kuwangaliwa, kwani waka...