Posts

Showing posts from June, 2023

RUSHWA MUHALI BADO NI GUMZO KWA KESI ZA UDHALILISHAJI

                           NA FATMA HAMAD PEMBA. Kuepo   kwa rushwa muhali katika jamii bado ni   changamoto   kubwa   inayopelekea kukwamisha   kwa kesi za udhalilishaji zisipate hatia. Akitoa ripoti   juu ya kesi za udhalilishaji mwendesha mashtaka wa serikali kutoka oisi ya mkurugenzi wa mashtaka   Chake   chake   Mussa Khamis katika kikao cha kamati ya kupinga udhalilishaji kilichofanyika ofisi za Tamwa Kisiwani Pemba. Amesema licha ya elimu inayotolewa kwa jamii ili kuacha muhali lakini bado hawaja kuwa tayari juu ya mapambano dhidi ya udhalilishaji. ‘’Bila ya mashirikiano ya pamoja hatuwezi tukafika pahala jamani tutabakia tunaimba tu   kila siku alisema PP Mussa. Aidha kwa upande mwengine alifahamisha kuwa kesi zinazowapa   changamoto katika uwendeshaji wake ni za watoto wa miaka 15, 16 na 17 hawataki kutoa ushirikiano   mahakamani. Baadhi ya wanakamati hiyo kutoka wilaya ya Mkoani wamekua wakivilalamikia vituo vya Polisi Mtambile na kengeja kuwa bado havijakuwa maki