Gharama za Uchaguzi zinavyokatisha ndoto za wanawake wanaogombea.
Wasema hali isiporekebishwa majimbo yataendelea kuwa magumu kwao Na Fatma Hama, Pemba ‘’NATAMANI kugombea tena uongozi katika uchaguzi ujao wa mwaka 2025, lakini kila nikifikiria gharama…nakata tamaa,’’ Hayo si maneno ya mtu mwengine bali ni ya mwanamama Tumu Mwalim Massoud mwenye miaka 40 mkaazi wa Wingwi Limani wilaya ya Micheweni Pemba, ambae aligombea uwakilishi Jimbo la Wingwi kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Mwanamama huyo kiu yake ni kuwa mwakilishi ili aweze kutetea haki za wananchi, ingawa anakumbuka gharama zilizomtoka katika uchaguzi wa mwaka 2020 na hatimae kushindwa katika kura. Anasema, kwa hali hiyo ndoto nyingi za wanawake wenye nia ya kugombea zitakatika na majimbo yataendelea kuongozwa na wanaume watupu, ambao kuna baadhi ya mambo yanaowahusu hawawezi kuyatetea. Ni mwaka wa 23 tangu Tumu aingie kwenye harakati za kisiasa, l...