Wajumbe wanawake kamati za shehia waleta mabadiliko
Shehia za Micheweni sera usawa ya kijinsia bado kitendawili
NA
FATMA HAMAD, PEMBA
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inatambua umuhimu wa kukuza usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake.
Uwepo wa sera ya Maendeleo ya Wanawake na
Jinsia ya mwaka 2000 na Mkakati wa Utekelezaji wake ya mwaka 2005,
unathibitisha dhamira ya wazi ya Serikali ya kukuza usawa wa kijinsia.
Lakini bado Sera hiyo haijatekelezwa ipasavyo, hili
limeonekana katika wilaya ya Micheweni, ambayo ina masheha 25, wakiwa wanaume
17 na wanawake wanane (8) pekee.
Hata kwa upande
wa wajumbe wa kamati za masheha utafiti umebaini kuwa, wapo 274, ingawa wanaume
ni 169 na wanawake ni 105 tu.
MASHEHA WENYEWE WANASEMAJE
Sheha wa Shumbavyamboni Time Omar Said anasema Sera
anaifahamu vizuri ndomana baada ya kupata uongozi akaweka wajumbe wanawake
Anasema kamati yake inawajumbe 10 watano wanawake na
wanaume watano.
Anasema anampango wa kuongeza idadi ya wajumbe wanawake
kwani wanaume ni wavivu kwenye kazi.
Sheha wa Wingwi Njuguni Hadia Omar Dadi, anaeleza kamati yake yenye wajumbe 10, wanaume ni sita
(6) na wanawake wanne (4).
Anasema bila ya kuwepo kiongozi mwanamke huwezi kuzijua
kero zinazo wakwaza wanawake, kwani ni vigumu kuelezea shida zao kwa wanaume.
‘’Siku zote mwanamke anaweza kufanya vizuri popote
atakapokuwepo, kwani mama ni mwenye roho ya huruma,’’anasema.
Suleiman Shaame Hamad sheha wa Sizini anasema kamati yake ina wajummbe 10, wanawake na wanaume wakiwa idadi sawa.
Anasema unapompa nafasi yoyote mwanamke ni rahisi, kufanikiwa, kwani wao ni wachapakazi na ni
washauri wazuri hasa katika nyanja za maendeleo.
‘’Binafsi nimeona
nilipowashirikisha wanawake katika kamati yangu, maendeleo yamepatikana, ukulinganisha
na hapo nyuma,’’anafafanua.
Hata kamati ya shehia ya Bopwe Wete, nayo ni mfano
mzuri wa utekelezaji wa sera, kwa kuwepo idadi ya wajumbe sawa ya watano kati
ya wanawake na wanaume.
shehia ya N’gambwa bado Sera imewapa kichogo maana
Shehia inawajumbe 12 lakini kuna wanawake wanne.
WANAKAMATI
‘’Mwanamke siku zote ndio mchapa kazi zaidi kuliko mwanamme, Ali Omar Ali mwanakamati ya
Sheha wa Wingwi Njuguni anasema Sera ya Maendeleo ya Jinsia imetekelezwa
ipasavyo katika Shehia yao, kwani hata Sheha wao ni mwanamke.
‘’Licha ya kua sheha wetu ni mwanamke lakini mabadiliko
tunayaona, hana ubaguzi wa chama, Rangi
wala Jinsia anafahamisha,’’.
Time Juma Said mkaazi wa Bopwe anasema licha ya kamati
yao kuwa na wajumbe wengi wanawake lakini haijawahi kupoteza kitu.
Anasema zamani kamati ilipokua na wajumbe wengi wanaume
ilikua na matatizo mengi ikiwemo utoro wa wanafunzi Maskulini.
KATIBA YA ZANZIBAR
Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, kifungu cha 10 (e) kimeleza
kila raia atakuwa na haki sawa, majukumu na fursa sawa kwa mujibu wa sheria.
Ijapokua katiba imeweka usawa kijinsia katika nyanja
mbali mbali ikwemo katika vyombo vya maamuzi, na pia nafasi za utendaji, lakini
usawa huo haujazingatiwa ipasavyo.
Kwani Zanzibar
inayo majimbo 50 ya uchaguzi, ingawa kwa
mujibu wa ripoti ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, wawakilishi wanaume ni 42 na
wanawake ni wanane (8) tu.
WANAHARAKATI
Afisa Mkuu wa mahusiano kutoka Chama cha wandishi wa
habari wanawake Tanzania Zanzibar -TAMWA Safia Ngalaphi, anasema licha ya kuwa
hawana utafiti rasmi lakini bado Sera ya Maendeleo ya Jamii na Jinsia,
haijatekelezeka ipasavyo.
‘’Tukiangalia
kwenye ngazi za shehia idadi ya masheha wanawake ni kidogo kwani ni 81 sawa na asilimi
20 kwenye
shehia 388 ya masheha wote Zanzibar,’’anaeleza.
Anaeleza kuwa wanatamani Sera yengetekelezwa, kwani siku
zote wanawake ni wapenda amani, wapenda maendeleo na waadilifu kwenye uongozi.
Hafidh Abdi Saidi kutoka jumuiya ya Utetezi wa
Kimazingira na Jinsia ‘’PEGAO ’’ ambapo yeye anasema kwa baadhi ya tasisi tayari wamekuwa na
uwelewa wa kuitekeleza Sera.
‘’Tukiangalia hata kwenye kamati ya Tume ya Uchaguzi ya
Bara ambayo imeundwa imezingatia usawa wa kijinsia,kwani ina wajumbe 19,
wanawake 12 na wanaume Saba tu.
Bimize Othman mkaazi wa Shumba mjini anasema katika
Shehia yao Sera imetelezeka maana hata
Sheha wao ni mwanamke.
‘’Tunajivunia kupata kiongozi huyu mwanamke kwani
tunauwezo wa kumueleza matatizo yetu ya ndani bila kumuonea aibu, ni tofauti
kama angekuepo mwanamme.
Omar Khatib Omar mkaazi wa wingwi njuguni anasema suala
la utekelezaji wa Sera ya Jinsia ni lazima kwani walipopata Sheha mwanamke maendeleo yalipatika.
‘’Ilikua kuna baadhi ya Vijiji havina huduma ya Maji
ila baada ya kuja Sheha mwanamke tumeondokana na shida hiyo,’’ ambapo kabla ya
yeye alikuepo mwaname anaeleza.
VIONGOZI
WA SERIKALI
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya anaeleza
kuwa, kiuhalisia mtendaji mkuu wa majukumu ya kazi ni mwanamke.
Anasema kama ofisi ya wilaya, watahakikisha kunakuwepo
na usawa kwa kamati zote kuanzia ngazi ya shehia hadi wilaya.
ilaya.
ATHARI
Kutokushirikishwa kwa wanawake katika tasisi kunaweza
kukapelekea kukosekana kwa fursa za kimaendeleo kwa baadhi ya makundi ya watu.
Mwanaisha Ali Masoud Mkuu wa Idara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na watoto Pemba anasema utekelezwaji wa
Sera unahitajika kuanzia hata kwenye ngazi ya familia.
‘’Tunataka kwamba kila alipo mwanamme na mwana mke
awepo kwani shida za wanawake anazijua mwanamke,’’anaeleza.
VIONGOZI
WA DINI
Sheikh Said Ahmed Mohamed kutoka Ofisi ya Mufti Pemba
anasema, uislamu umemruhusu mwanamke
kushiriki nafasi ya uongozi, anayoiweza kwa mujibu wa dini
inavyoelekeza.
Mchungaji Yohana Ali Mfundo wa Machomane Chake chake,
amefahamisha kuwa katika dini yao hakuzuiwa mwanamke asishiriki kwenye mamuzi,
ilimradi afuate masharti yaliopo.
NYARAKA
Tamko la Jumuiya ya Maendeleo la nchi za Kusini mwa
Afrika (SADC) la mwaka 2005 na itifaki ya SADC ya Jinsia na maendeleo la mwaka
2008, ni kuhakikisha kuna usawa wa kijinsia katika ngazi zote za maamuzi.
Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020/2025 ni
kuhakikisha inaimarisha usimamizi wa utendaji wa masuala mtambuka katika mamlaka
za Serikali za mitaa kama usawa wa kijinsia.
Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na
watoto Zanzibar ya mwaka 2024/2025 imebainisha kuwa, tafiti zinaonesha kuwa nchi
zinazozingatia usawa wa kijinsia zimeweza kuimarika kiuchumi kwa kasi kuliko nchi
ambazo hazizingatii usawa huo.
NINI
KIFANYIKE?
Sheha wa Bopwe,
anasema ni vyema na masheha wengine kuiga mfano wake kuhakikisha wanaweka uongozi sawa, kati ya
wanawake na wanaume.

Comments
Post a Comment