Posts

Showing posts from May, 2024

WANAHABARI, WADAU WAOMBA VIFUNGU VINAVYOMINYA UHURU WA HABARI VIREKEBISHWE

Image
                                                NA FATMA HAMAD,PEMBA KILA baada ya miaka 10 sheria huwa zinahitaji kubadilishwa ili kuondosha mapungufu ya vifungu ambavyo vitakua haviendani na utekelezaji wa sheria hiyo.   Ijapo kuwa wakati mwengine sio lazima kusubiriwe hadi itimie miaka 10 ndio   iweze kufanyiwa marekebisho. Na hii itasaidia kuweka sawa vifungu vyenye mapungufu ili viweze kuendana na muda na mazingira ya sasa. Lakini tukiangalia sheria ya Usajili wa Uwakala wa habari, Magazeti na Vitabu namba 5 ya mwaka 1988 iliyofanywa marekebisho na Sheria Namba 8 ya mwaka 1997, haiendani na mazingira ya sasa kwani ni  kongwe hivyo inahitajika ifanyiwe marekebisho. Takriban ni miaka 26 tangu Sheria hiyo kufanyiwa marekebisho ingawa bado baadhi ya vifungu vyake vina mapungufu ambavyo vinaminya uhuru habari. Miongoni mwa vifungu hivyo ni kifungu cha 30 kinachompa   mamlaka makubwa   Waziri kiasi ambacho kinaminya uhuru wa habari pamoja na kifungu cha 27[1], 27[2].   A

DK MWINYI AWAFURAHISHA WANANCHI PEMBA

Image
      *RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameeleza nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuendeleza ujenzi wa miundombinu imara kwa Sekta za Maendeleo nchini.*  Dk. Mwinyi ameeleza hayo uwanja wa Jamuhuri wa Skuli ya Sekondari Utaani Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba, alipofungua skuli ya Sekondari ya wanawake ya Ghorofa tatu iliyojengwa upya na serikali baada ya kupata ajali ya kuunga moto na kuteketeza kila kitu Mwezi Machi mwaka 2022.  Alisema, ujenzi wa skuli hiyo ni utekelezaji wa ahadi ya serikali iliyoitoa baada ya tukio la moto lililoteketeza skuli ya awali iliyokuwa na madasa 11 na kuahidi kujenga skuli bora zaidi ambayo kwasasa ina madarasa 41.  Aidha, Rais Dk. Mwinyi ameahidi kujenga dahalia kubwa ya kisasa itakayoendana na hadhi ya skuli hiyo.  Katika kuboresha haiba njema ya mandhari mpya ya eneo la skuli hiyo, Rais Dk. Mwinyi ameiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kusimamia ujenzi uliobakia wa ukumbi wa mi