WANDISHI WA HABARI WAHIMIZWA KUANDIKA HABARI ZA VIJIJINI.
Afisa mdhamini wizara ya habri Vijana na Michezo Salum Ubwa amewataka wandishi wa habari kujikita zaid Vijijini katika kuandika habari zao ili kuibua matatizo yanayo wakabili wananchi wa maeneo hayo. Hayo ameyasema katika Kongamano la uhuru wa kujieleza upatikanaji wa habari, mitandao ya kijamii na uandaaji wa maudhui kwa vijana na majukwaa ya maendeleo kwa vijana huko Camail Chake chake Pemba. Amesema vyombo vya habari ndio msemaji wa wasio na sauti, hivyo ni budi kwa wandishi wa habari kujitoa na kujituma ili kuona wananchi wa vijijini nawao wanapata fursa ya kuzungumza na vyombo vya habari kutoa kero zao na mamlaka husika na kuona wana zitekeleza. ‘’Wandishi msiishie tu mjini nendeni vijijini kuna kero nyingi zinawakumba wananchi’’ Alisema afisa mdhamini. Amesema wananchi wengi wa vijijini wanaendelea kuishi katika matatizo kutokana na kukosa taluma na taratibu za ufuatiliaji wa shida zao kwa vyombo husika jambo ambalo linapelekea kukosa haki zao.