Serekali kutoa adhabu kali kwa wafanyaji wa vitendo vya udhalilishaji.


 Mama mmoja amevunja ukimya na kuiomba Serikali kutoa hukumu kali kwa watu wanaofanya ukatili ya kuwalawiti na kuwabaka watoto na wanawake ili kukomesha vitendo hivyo visitokea tena.

Kauli ya mama huyo imefuatia baada ya tukio la kuhudhunisha la kuingiliwa kinyume na maumbile kwa mtoto wa mika 5 na kijana Mussa Saleh  Ali mwenye umri wa 16 huko wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa mama wa mtoto huyo amesema tukio la kufanyiwa kitendo hicho mwanawe lilitokea wakati alipokwenda jisaidia vichakani majira ya saa 10 jioni baada ya nyumba yao kutokuwa na choo na kurudi kwao saa 12 jioni akitokwa na mchozi.

Amesema alipo muhoji alimwambia alichomwa na ujiti, lakini mwisho wa siku alipombana zaidi na kumtishia  ndipo alisema kuwa  Mussa ndie aliyemfanya kitendo  kilichomtoa damu huku akimuamuru asiseme jambo hilo kwa mtu yeyote na akisema ataweza kumfanyia kitu kibaya.

‘’Mimi nilikua sina habari nikaambiwa na wenzake mbona hajarudi choni hapo nikaamua kumtafuta nikamuona anatoka vichakani akiwa analia’’ Alisema mama mtoto.

Aidha amesema kuwa baada ya kumuona hivyo alimchukua na kukimbilia kituo cha Polisi kutoa taarifa, na baadae kuripoti kuelekea Hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kuambiwa tayari  mtoto ameshaharibiwa.

Ameeleza kuwa tukio hili limemtia huzuni kwani  mtuhumiwa huyo ambae amemfanyia  mwanawe unyama huo ni ndugu wa familia ni [mtoto wa dada yake] waliozaliwa na pamoja.

‘’Sikufikiria kama mototo wa dadangu anaweza kumfanyia ukatili mwanangu’’ amesema mama motto.

Baba wa motto huyo ambae amefanyiwa udhalilishaji amesema hayuko tayari kukubali kupokea rushwa ya aina yoyote ili asamehe kesi bali atashirikiana na vyombo vya sheria mpaka haki ya mtoto wake ipatikane.

‘’Nikikubali kupokea rushwa ataendelea kuwadhalilisha na wengine, sikotayari na hilo’’ Alisema baba mzazi.

Kwa upande wa Babu wa aliedhalilishwa amesema licha ya mtuhumiwa huyo kuwa ni mjuu wake lakini  hatokubali kufanya suluhu, bali aiomba serikali ichukue mkondo wake wa sheria.

Mapema sheha wa shehiya hiyo Maryam Mjawiri Juma ameitaka jamii kuwa karibu na watoto wao huku akiwataka kuendelea na ujasiri wa kuripoti matukio ya udhalilishaji katika vyombo vya sheria pindi yanapotokezea.



Mratibu wa wanawake na watoto   amesema mtoto wa miaka  5 kufanyiwa udhalilishaji ni mtihani mkubwa hivyo ni vyema Jamii kuwa na mashirikiano na vyombo vya kisheria kuwafichua wahalifu ili kuondosha janga hilo.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Kaskazini Pemba Juma Sadi amekiri kutokea kwa tukio hilo, la kinyama ambapo kwa sasa mtuhumiwa huyo tayari yupo katika mikono ya Jeshi la Polisi.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.