Posts

Showing posts from October, 2021

WANDISHI WATAKIWA KUIHAMASISHA JAMII JUU YA UMUHIMU WA CHANJO YA UVIKO 19

Image
  AFISA MdhaminiWizarayaAfyausatawiwaJamiijinsiaWazeenaWatotoPemba,Yakob Mohamed Shoka amewataka waandishi wa Habari kutumia nafasin zao katika kuielimisha jamii kujitokeza kupatachanjo ya kujikinga na uviko 19. Shoka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika hafla ya mafunzo ya uhamasishaji wa uchomaji wa chanjo uliofanyika Maabara kuu ya jamii   Kisiwani Pemba. Amesema waandishi wananafasi kubwa ya kuifikia jamii kwa haraka katika kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kupata chanjo ya kujikinga na Virusi vya korona. Maratib wa Huduma za Chanjo Kisiwani hapa Bakari Hamad amesema Chanjohiyo inatolewa katika Hosptali na Vituo mbalimbali vya Afya ikiwemo Hospital ya Micheweni, Wete Chakechake Pamoja na Abdala Mzee Mkoani ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma hiyo.   Nae Afisa muuguzi wakitengo Cha Chanjo Zanzibar Dr Huzuna Abd-rahman amewaomba wananchi kulipauzito hasa wale wenyemaradhi yasukari, presha kutokuwanyuma katika zoezi hilo. Katika haf

kijana huyu mwenye ulemavu wa viungo ashindwa kwenda skuli kwa kukosa kibaskeli cha maringi mawili

Image
Licha ya juhudi zinazochukuliwa na Serikali pamoja na Asasi mbali ili kuona  watu wenye ulemavu na wao wanapata haki  zao stahiki, lakini bado watu hao wanaendelea kukumbana na changamoto kadhaa na kupelekea kudumaa kwa maendeleo yao. Hayo yamebainika kwa  Kijana Anifu Jeilani Issa  mwenye ulemavu wa Viungo  (14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la tano Skuli ya Msingi Ole Wilaya ya Chake Chake Pemba, kushindwa kuhudhuria Skuli kwa kukosa Kibaskeli cha magurudumu mawili. Akizungumza kwa masikitiko  Mama Mzazi wa Mtoto huyo huko Nyumbani kwake Ole Mihogoni   amsema ni Zaidi ya miezi minne hivi sasa mototo wake Anifu hajahudhuria Skuli kuungana na wenzake kusoma kufuatia changamoto hiyo.  ‘’ alikua nacho kigari lakini sasahivi kimeharibika, jambo ambalo linapelekea kukosa masomo yake’’ Alisema mama mzazi  Hivyo mama huyo amewaomba wahisani pamoja na wasamaria wema kupatiwa msaada wa kigari ili kuweza kushiriki kikamilifu katika masomo yake kwa vile hivi sasa anashindwa kuhudhuria kwa  kuko

WANDISHI WATAKIWA KUWA WALIMU WAZURI KWA JAMII JUU YA UTUNZAJI WA AMANI

Image
Wandishi wa habari wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuielimisha Jamii kujiepusha na migogoro   amboyo inaweza kupelekea uvunjifu wa Amani. Wito huo umetolewa na mwenyekiti wa jumuia ya Wandishi wa habari Kisiwani Pemba [PPC] Bakar Mussa Juma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili   juu ya utekwelezaji wa mradi wa Sauti yangu, Amani yangu ndio khatma yangu kwa wandhishi wa habari huko Gombani Chake chake. Amesema wandishi wa habari wanamchango mkubwa wa kuisaidia   jamii, hivyo ni budi kutumia taaluma yao kwa kuielimisha juu ya   athari zinazojitokeza wakati kunapokua na migogo. ‘’ Nyinyi wandishi mnaaminika katika jamii, hivyo ipeni elimu jamii ili isiwe katika migogoro na badalayake ibaki salama’’ Alisema mwenyekiti PPC. Aidha amesema bila ya kuepo kwa Amani hakuna lolote linaloendelea, hivyo ni vyema watu wanapokoseana kuvumiliana na kusuluhishana jambo ambalo litapelekea kuwepo kwa maendeleo na kudumu kwa Amani Nchi iliyopo sasa. Kwa upande wake mwenyekiti mstaafu wajumuia

JUMUIA YA WANDISHI WA HABARI YAZINDUA MRADI WA SAUTI YANGU , MANI YANGU NDIO KHATMA YANGU

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA. WaandishiwaHabariKisiwani Pemba,wamesema kuwepo kwa mradi wa Sautiyangu Amani yanguHatma yanguutawezakuwasadiakatikakuandikahabarizinazolengamaswalayautatuziwamigogoro. Wakizungumza Mara baadayauzinduziwaMradihuohukokatikaukumbiwaTumeyaUkimwiKisiwaniPemba,wamesemamradiahuoutawawezeshanamnayakuielimishajamiiumuhimuwakutunza Amani. ‘’kupitiamradihuusisiwandishiwahabariutatusaidiakatikakuandikahabarizamigogoro’’Walisemawandishi. Kwaupande wake mwandishi Hassan Mselemkutokabaharifmamesemamaranyingivijanandiowanaotumiliwavibayakatikakuvuruga Amani yaNchi, hivyoatahakikishaanandikahabarizitakazotoajuuyaumuhimuwa Amani katikaJamii. MapememaMwenyekitiwaJumiyayaWaandishiwaHabariPembaPresiClabuKisiwanihapaBakariMussaJumaamesemamradihuoutasadiakuongezauwelewajuuyaumuhimuwakutunza Amani hasakatikakipindi cha Uchaguzi. ‘’Lengo la mradihuonikuwajengawandishiwahabarikutoaelimukwajamiiilikujiepushanamigogoro’’ AlisemaMwenyekiti. MradiwaSautiyangu Amani yanguhatmayanguulio

MKE WA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS AKABIDHI VIFAA VYA HUDUMA YA MAMA NA MTOTO KATIKA HOSPITALI YA VITONGOJI

Image
  MKE wa Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Mama Zainab Kombo Shaib, ametoa wito kwa mamlaka zote pamoja na asasi za kiraia, kuimarisha afya ya mama na mtoto, ili kujenga ustawi bora wa jamii, utakaochangia maendeleo ya nchi.   Mama Zainab aliyasema hayo leo katika ziara yake, alipotembelea Hospitali ya Vitongoji, Wilaya ya Chake Chake, Mkoa wa Kusini Pemba.   Alisema afya ya mama na mtoto ni sehemu muhimu ya msingi wa ustawi wa jamii, unaolenga kuzalisha na kuendeleza nguvu kazi ya Taifa, na hatimaye kufanikisha juhudi za kujiletea maendeleo.   "Afya zikiwa vizuri hata uzalishaji unaongezeka, hivyo ni vyema kuzitumia rasilimali tulizonazo kwa uangalifu katika kutoa huduma bora za kijamii ambazo ni pamoja na afya ya mama na mtoto," amesema Mama Zainab.    Akitoa nasaha zake mbele ya madaktari na wahudumu wa hospitali hiyo, Mama Zainab ameahidi kupaza sauti kwa wadau wa afya ili kusaidia kuzitatua changamoto, zikiwemo za uhaba wa vifaa,

WANAWAKE WATAKIWA KUSHIRIKIANA ILI WAWEZE KUJILETEA MABADILIKO

Image
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,  Mama Zainab Kombo Shaib, ametoa wito kwa wanawake nchini kushikamana ili kuweza kujikomboa kutokana na ukubwa wa wimbi la changamoto zinazowakabili    Mama Zainab ametoa wito huo huko, Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba, wakati   akizungumza   na akinamama wa ACT-Wazalendo wa Mikoa miwili kichama, ya Wete na Micheweni kisiwani humo.   Alisema ukombozi wa mwanamke ni sawa na ukombozi wa jamii yote na njia ya matumaini kuelekea maendeleo ya Taifa zima   Alifahamisha kuwa matumaini na mafanikio ya ukombozi wa kweli wa mwanamke hayawezi kufikiwa pindipo akinamama wenyewe watashindwa kujitambua, kushikamana na kusaidiana.   "Wanawake ni wengi, na  nguvu yetu ni kubwa sana, tukiungana,tukishirikiana pamoja tukaacha makundi na kuchukiana tutafika mbali na tutalisaidia taifa katika kufikia ukombozi" alieleza Mama Zainab.   Mama Zainab aliwataka wanachama hao kuendeleza uwajibikaji katika shughuli za chama ili kuisimamisha dhamira ya

JAMII JATAKIWA KURUDISHA MALEZI YA PAMOJA KATIKA KULEA WATOTO WAO

 MKUU wa Wilaya ya Wete Hamad Omar Bakar ameitaka jamii kushirikiana pamoja katika kupinga  vitendo vya udhalilishaji ambavyo vimekuwa vikiongezeka siku hadi siku. Alisema kuwa kwa mujibu zilizotolewa na Wizara ya afya na Ustawi wa jamii imebainisha kuwa Shehia ya Kizimbani kwa Wilaya ya Wete imekuwa ikiongoza kwa vitendo vya udhalilishaji. Mkuu huyo wa Wilaya aliyasema hayo huko katika ukumbi wa Skuli ya Sekondari Idrisa Abdulwakil Kizimbani Wete, wakati alipokuwa akizungumza na Kamati mbali mbali zilizomo katika Shehia ya Kizimbani. Alieleza kuwa Shehia ya Kizimbani ni miongoni mwa Shehia 36 zilizomo katika Wilaya ya Wete ambayo imekuwa ikitajika sana kuongoza katika vitendo vya udhalilishaji ndani ya Wilaya hiyo. "Tumeitana hapa ili tuweze kujadiliana au kubuni mbinu zipi ambazo tutaweza kuzitumia ili kuondosha tatizo hili la unyanyasi katika Shehia yetu hii ya Kizimbani kwani imekuwa ni Jambo la aibu sana," alisema Mkuu huyo wa Wilaya. Mapema Mkuu huyo wa Wilaya aliwataka

UMASKINI WAPELEKEA WATOTO 6 WENYE ULEMAVU WA AKILI NA VIUNGO KUSHINDWA KUPATA HUDUMA MUHIMU ZA KIJAMII

Image
Wazazi wa watoto sita wenye ulemavu wa akili na viungo huko Kinyasini Mikarafuuni Wilaya ya Wete Pemba wamewaomba wasamaria wema kuwapatia msaada  ili kuweza kuwahudumia watoto wao, kwani kwa sasa wanashindwa kutokana na hali ngumu waliyonao jambo lililosababisha  kuwakatisha masomo. Akizungumza na wandishi wa habari huko nyumbani kwake  Kinyasini Wete  baba mzazi wa watoto hao Saleh Juma Saleh ambapo ameanza kwa kueleza faraja  alioipata huko nyuma wakati watoto hao wakiwa ni wadogo kwa kufikwa na baadhi ya wahisani pamoja na viongozi wa serikali. ‘’Kipindi cha nyuma nashukuru walikuja watu wengi ikiwemo Serikali kuniona hali yangu na kunifariji, ila kwa sasa ni nadra na hali imezidi kuwa ngumu kwangu, alisema baba watoto. Amefahamisha kuwa awali walikua wanasoma Shule ila kwa sasahivi wameshindwa kuendelea tena kutokana na ugumu wa maisha. ‘’Nimewakatisha masomo kutokana na uwezo,  Gari ipo ila sina mafuta ya kutia  kila siku na kuwapelekea shule,  na hivi saivi gari imelala bandani

RUSHWA BADO NI TATIZO KWA WAGOMBEA WANAWAKE KISIWANI PEMBA.

Image
Wanawake wagombea Kisiwani Pemba wapaza sauti zao kwa vyombo vya habari juu ya Kuepo kwa rushwa katika vyama vya siasa   kipindi cha uchaguzi mkuu, kikwazo ambacho kinapelekea wanawake   hao   kushindwa kufikia malengo yao. Akizungumza  kwa masikitiko Hadia Omari Dadi katika mkutano wa uhamasishaji wa mwanamke kugombea nafasi za uongozi, huko Wingwi wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba alisema  unapofikia wakati wa uchaguzi suala la rushwa hujitokeza kwa wingi katika vyama jambo ambalo linawakosesha wanawake wenye kipato duni kushindwa kujinyakulia nafasi mbalimbalizauongozimajimboni. Alisema inaonekana wengi wanaopata nafasi hizo ni wale wenye nacho,auwaleambaotayariwalishakaakwenyeuongozikwakipinchama. ‘’Mimi mwenyewe binafsi nishagombea mara tatu ila kwa sababu ni masikini, sina pesa nimeshindwakupatanafasiyoyoteilekutokanasinauwezo,’’Alisemabia. Alifahamisha kuwa Rushwa ni adui mkubwa anekwamisha maendeleo, hivyo tunaishauri  Serikali  ya Mapinduzi kujipanga upya kat