WANDISHI WATAKIWA KUWA WALIMU WAZURI KWA JAMII JUU YA UTUNZAJI WA AMANI
Wandishi wa habari wametakiwa kuwa mstari wa mbele kuielimisha Jamii kujiepusha na migogoro amboyo inaweza kupelekea uvunjifu wa Amani.
Wito
huo umetolewa na mwenyekiti wa jumuia ya Wandishi wa habari Kisiwani Pemba
[PPC] Bakar Mussa Juma wakati akifungua mafunzo ya siku mbili juu ya utekwelezaji wa mradi wa Sauti yangu,
Amani yangu ndio khatma yangu kwa wandhishi wa habari huko Gombani Chake chake.
Amesema
wandishi wa habari wanamchango mkubwa wa kuisaidia jamii, hivyo ni budi kutumia taaluma yao kwa
kuielimisha juu ya athari zinazojitokeza
wakati kunapokua na migogo.
‘’
Nyinyi wandishi mnaaminika katika jamii, hivyo ipeni elimu jamii ili isiwe
katika migogoro na badalayake ibaki salama’’ Alisema mwenyekiti PPC.
Aidha
amesema bila ya kuepo kwa Amani hakuna lolote linaloendelea, hivyo ni vyema watu
wanapokoseana kuvumiliana na kusuluhishana jambo ambalo litapelekea kuwepo kwa
maendeleo na kudumu kwa Amani Nchi iliyopo sasa.
Kwa
upande wake mwenyekiti mstaafu wajumuia ya wandishi wa habari [PPC] Said Mohd Ali
amewaasa wandishi wa habari kuepuka kuandika habari za uchochezi ambazo
zinaweza zikaleta mfarakano na mivutano katika Jamii.
‘’Wandhi
andikeni habari zenye ukweli na zenye faida kwa jamii, msiwe chanzo cha
migogoro’’Alisema mwenyekiti mstaafu.
Ali
Masoud Kombo mwandishi kutoka redio jamii micheweni ambae ni miongoni mwa
waliohudhuria mafunzo hayo amewataka wandishi wenzake wajiamini na wasiwe na woga wakati wanapokua katika majukumu yao
ilimradi tu wafuate Miko, Kanuni na Madili ya kazi yao.
Comments
Post a Comment