Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.
NA FATMA HAMAD PEMBA. Wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu wamekumbushwa kuacha tabia ya kuwanyanyapaa na kuwafungia ndani watoto hao, kwani kufanya hivyo ni udhalilishaji kwao. Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Tumbe Mashariki katika mkutano maalumu Mkuu wa Polisi Jamii mkoa wa Kaskazini Abdala Majid Haji amesema wapo baadhi ya watu wamekuwa na itikadi potofu ya kuwachukulia watoto wenye ulemavu kama ni watu wasio na faida na badalayake huishia kuwafungia majumbani. ‘’Baadhi yetu hapa tunao watoto wetu wenye ulemavu tumewafungia tu ndani, hawatoki njee eti tunahofia jamii itatucheka,alisema. Alisema Watoto wenye ulemavu nawao ni binadamu kama wengine wanastahiki kupata haki na fursa mbali mbali kama vile Elimu, Afya,Ajira. Alieleza kuwa ni wakati kwa wazazi wanaoishi na watoto wenye ulemavu kubadilika na kuhakikisha wanatoa matunzo sawa na wenzao wengine wasio na ulemavu. Alifahamisha udhalilis