WANDISHI WA HABARI WANAWAKE WAPEWA MBINU

 

                                NA FATMA HAMAD,PEMBA

Wandishi wa habari  wametakiwa kuitumia   mitandao ya kijamii  kwa kufuata sheria za mtandaoni wakati wanaporusha habari zao ili kuepuka changamoto mbali mbali zinazojitokeza ikiwemo  unyayasaji.

Hayo yamesemwa na Mtalamu wa mambo ya kidijitali kutoka shirika la Pen Amercan Cecilia Maundu wakati akizungumza na wandishi wa habari wanawake kutoka vyombo mbali mbali Zanzibar katika mafunzo yaliofanyika kwa njia ya mtandao [ZOOM]  juu ya kujilinda dhidi ya Unyanyasaji mtandaoni.

Amesema suala la unyanyasaji katika mitandao limeongezeka,  hivyo ni wakati sasa wandishi wa habari wanawake kuhakikisha wanafuata Sheria na masharti  ipasavyo wakati wanapotuma kazi zao katika mitandao ya kijamii.

‘’Tumeona kwamba Wanawake ndio wathirika wakubwa  wa udhalilishaji  katika mitandao, hivyo tuweni makini jamani katika kutumia kwetu mitandao hiyo, alisema.

Aidha Alifahamisha kuwa sio busara kutumiana picha za uchi  kwani ni njia moja ya kuwarahisishia watu kukufanyia unyanyasaji.

‘’Jamani tujiepusheni kutumiana picha zetu tukiwa utupu hatakama ni mume wako,mke wako, mpenizi wako,alifahamisha.

Alisema lengo la mafunzo hayo kwa wandishi wa habari wanawake ni kuwapa taluma  waweze kuitumia mitandao ya kijamii ipasavyo ili waepukane na unyasasaji.

Akichangia  katika mkutano huo mwandishi wa habari kutoka Chama cha Wandishi wa habari Wanawake  Tanzania Zanzibar [TAMWA] Khairat Haji  aliwataka wandishi wa habari wenzake kuepuka kuweka vitu vyao binafsi [vya siri] ambavyo vinahusu familia zao, ili kuepuka kudukuliwa tarifa zako.

Nao badhi ya washiriki wengine walilipongeza Shirika la Pen Amerca kwa kuwapatia mafunzo hayo ambayo yatakuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko katika utumiaji wao wa mitandao ya kijamii.

Hivyo wameliomba shirika hilo kuendelea kuwapa taluma hiyo jambo ambalo litawasaidia kuwa na uwangalifu wa hali ya juu wakati wanapotumia mitandao ya kijamii katika utekelezaji wa majukumu yao ili waweze kuepukana na Unyanyasaji.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.