BAADA YA BLOG YA PEMBA YA LEO KUIBUA KERO YA MWALIMU WA MADRASA MWENYE ULEMAVU KOKOSA SEHEMU SALAMA YA KUSOMESHEA SASA APATA UFADHILI WA KUJENGEWA.
BAADA YA BLOG YA PEMBA YA LEO KUCHAPISHA MAKALA -Mwalimu mwenye ulemavu wa viungo ajengewa mdarassa Shumba vyamboni -Aibuka kuushukuru mtandao wa pemba ya leo, mfadhili, wanafunzi wasema jambo FATMA HAMAD, PEMBA JUNE 24 , mwaka 2022, Blog ya pemba ya leo, lilichapisha makala, ikielezea changamoto za ukosefu wa madrassa ya kisasa ya mwalimu wa madrasa mwenye ulemavu wa viungo. Mwalimu huyo Saada Khamis Hamad wa Shumba vyamboni wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba, akikabiliwa na changamoto ya ukosefu sehemu rafiki na salama ya kusomeshea wanafunzi wake. Ndoto zake za kupata madrassa ya kisasa kwa ajili ya kufundishia wanafunzi wake, hakuwa nayo kabisa kwenye akili yake, hasa kwa vile alishasomesha miaka zaidi ya minne katika mazingira magumu. Kwa kweli alikua na kilio cha siku nyingi, cha kupata ufadhili wa kujengewa madrasa, ndipo mwandishi wa makala kupitia blog ya pemba ya leo Pemba, alipochapisha makala yake na kisha wafadhili kucho moza . Nilikua sin