WANAHARAKATI WAPEWA MBIN
NA FATMA
HAMAD PEMBA.
Wanaharakati
pamoja na asasi mbali mbali za kiraia zimekumbushwa kuwa mstari wa mbele kuwasimamia na kuwatetea wanawake
na watoto wakati wanapopatwa na
matatatizo ikiwemo udhalilishwaji na
utelekezwaji ili kuona wanapata haki zao.
Ukumbusho
huo umetolewa na mkuu wa kituo cha polisi micheweni Said Khamis Juma katika kongamano la madhimisho
ya asasi za kiraia ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa
wanawake na watoto huko micheweni kisiwani Pemba.
Amesema
asasi za kiraia zinatambulika kisheria
na kimataifa hivyo ni wakati wa kujitowa na kuwatetea wanawake na watoto wanapodhalilishwa
ili kuona hatua zinachukuliwa jambo
ambalo litapunguza vitendo hivyo.
‘’Asasi za
kiraia mnanafasi kubwa hivyo ni wajibu wenu kuwatetea na kuhakikisha wanawake na watoto wanapata haki zao zinazostahiki
wakati zinapovunjwa’’alisema mkuu wa kituo.
Alieleza
kuwa udhalilishaji si jambo la kufanyiwa doria kwani maranyingi hufanywa na
watu wa karibu kwenye familia bali ni suala
linalohitaji ushirikiano wa kila mmoja iwe jamii, Serikali na hata asasi za
kirai kuhakikisha wahalifu wa matukio
hayo wanafichuliwa na kupelekwa kwenye
vyombo vya sheria.
‘’Udhalilishaji
sio jambo la kuchezea jamani hivyo ni lazima
kila mmoja kwa nafasi yake atoe ushirikiano wa hali ya juu ili kuondosha
tatizo hili linalokatisha ndoto za wanawake na watoto’’ alisema kwa huzuni mkuu
wa kituo.
Akitoa
nasaha katika kongamano hilo mratibu wa chama cha wandishi wa habari wanawake
Tanzania tamwa ofisi ya Pemba Fathiya Mussa Said amesema wakati umefika kwa
wazazi kukaa chini na watoto wao wa jinsia zote bila ya aibu kuwafundisha
madhara ya udhalilishaji pamoja na
kujitambua ili waepuke kujingiza
katika janga hilo.
Nao
washiriki wa kongamano hilo wamesema nivyema wanaharakati kupita kijiji hadi
kijiji kuendelea kuielimisha jamii kwani imeonekana bado wapo wazazi wamekua
wakikwepa majukumu yao kwenye fanilia na kusababisha kutokea kwa udhalilishaji
kwa wanawake na watoto.
Comments
Post a Comment