Posts

Showing posts from April, 2021

MABARAZA YA YATAKIWA KUCHAGUA VIONGOZI WAPYA WENYE SIFA

Image
Wajumbe wa mabaraza ya Vijana Zanzibar wametakiwa kuchagua viongozi imara ambao wataendesha vyema mabaraza hayo. Akizungumza na wajumbe wa mabaraza ya vijana kisiwani Pemba Afisa mdhamini Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Salum Ubwa Nassor katika mkutano wa tathimini wa baraza hilo tangu lilipoanzishwa mwaka 2016 hadi 2021 huko Gombani Chake chake Pemba. Amesema bila ya viongozi wenye sifa hawawezi kulifanya baraza kufikia katika maendeleo yaliokusudiwa katika kuanzishwa kwake. ‘’Niwaombe wajumbe mliopo kwenye baraza na mliostafu kutafuta wenye viti na makamo wapya ambao wataliendeleza baraza hilo’’ amesema mdhamin ubwa. Akifafanua kua viongozi wa mabaraza yaliopita walifanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani waliweza kuongeza vijana wengi katika mabaraza yao. Kwa upande wake mwenyekiti wa baraza la Vijana Zanziba Khamis Kheri Makoti amesema wameamua kufanya tathmini ya mabaraza ya vijana kwa mujibu wa sheria ya kuanzishwa kwake katika kipindi chote cha uongozi wao tokea

TALAKA ZACHANGIA UDHALILISHAJI KWA WATOTO

Image
Kukosekana kwa Malezi ya pamoja kati ya Baba na Mama ni chanzo kikubwa kinachopelekea Watoto kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ikiwemo Ulawiti na Ubakaji. Akizungumza na Pemba ya leo Katibu wa kamati ya Madili kupitia baraza la Tasisi za Kislamu Zanzibar Abdala Mnubi Abasi amesema imebainika kuwa wanandoa wengi wanapoachana mzigo mkubwa wa malezi humuangukia mama peke yake hali ambayo kunakosekana kwa huduma bora kwa Watoto. Amesema kukosekana kwa malezi ya pamoja ya Baba na Mama watoto hukosa  matunzo stahiki na kuamua kujiajiri wenyewe hali ambayo inasababisha kufanyiwa udhalilishaji. ‘’Inapovunjika ndoa   Watoto husambaratika kwani mababa hawatoi tena huduma’’, Alisema katibu wa madili. Amesema imebainika kuwa wengi wafanywaji wa matukio hayo ni watoto ambao wamekosa malezi ya pamoja kutokana na wazazi wao kuachana. Katibu huo amewataka wanajamii kuwa na subra wakati inapotokezea migogoro ya kifamilia na kutafuta suluhu mbadala ili kuepusha talaka za ovyo ovyo jambo ambalo litawaf

WANANCHI WAHIMIZWA KUWAPELEKA WATOTO VITUO VYA AFYA KUPATA CHANJO

Image
Wizara ya Afya Zanzibar imewataka Wananchi kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao katika Vituo vya Afya ili kupata chanjo jambo ambalo litawakinga Watoto na maradhi mbali mbali ya mambukizi ikiwemo Pepopunda na Kifaduro. Akizungumza na Wandishi wa habari huko ukumbi wa Maabara Chake chake Pemba Afisa Mdhamini wizara ya Afya Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Yakoub Mohd Shoka amesema zoezi la utoaji wa chanjo litanza rasmi tarehe 26 hadi 30 mwezi huu katika Vituo vyote vya Afya vilivyomo wilaya zote Visiwani hapa. Amesema   kila mwisho wa   mwezi wa Nne ya kila mwaka, ni wiki ya chanjo ya Afrika ambapo kwa Zanzibar   wizara ya Afya huadhimisha   zoezi la utoaji wa chanjo za kawaida kwa Watoto na akinamama ili kua na jamii isio na mambukizi ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ‘’Chanjo huweka Jamii pamoja’’. Amesema lengo la Chanjo hizo ni kuhakikisha Watoto wote wanapatiwa, ili waweze kuondokana na maradhi hatarishi ikiwemo Saratani ya mlango wa kizazi, Polio, kifua kikuu, Suru

KOCHA wa timu ya Waawi Star Kasim Ali Kasim amesema atautumia mfungo wa ramadhani kwa kukifua kikosi chake ili kiwefiti katika michano ya ligi daraja la kwanza kanda ya Pemba,itayoendelea tena mara baada ya mfungo wa Mwezimtukufu wa ramadhani.

  KOCHA wa timu ya Waawi Star Kasim Ali Kasim amesema atautumia mfungo wa ramadhani kwa kukifua kikosi chake ili kiwefiti   katika michano ya ligi daraja la kwanza kanda ya Pemba,itayoendelea tena mara baada ya mfungo wa Mwezimtukufu wa ramadhani. Wawi Star ambayo ilishawahi kushiriki   ligi kuu ya Zanzibar, msimu wa mwaka juzi iliyaanza mashindano hayo kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mkoroshoni United katika   mchezo uliopigwa uwanja wa Gombani Kisiwani hapa. Akizungumza na Mwanaspoti Kocha huyo alisema licha kuwa Vijana wake wapo kwenye swaumu lakini atakitumia kipindi cha mapunziko ya ligi kwa kufanya mazoezi ya kufa mtu kuona wanafanya vizuri kwenye mzunguko wa pili. Alisema katika mzunguko uliopita aliona udhaifu mkubwa kwenye   kikosi chake hasa katika sehemu ya umaliziaji kiasi cha kumfanya kocha huyo kuamua   kuutumia mwezi huu wa mfungo kukiandaa kikosi chake. ‘’Kkipindi hichi cha ramadhani hatutolala tutahamasishana kufanya mazoezi kuona yale mapungufu yaliyojitokeza kati

TIMU ZA LIGI DARAJA LA KWANZA KISIWANI PEMBA ZATAKIWA KJIANDA VIZURI ILI KUKABILIANA NA MZUNGUKO WA PILI BAADA YA MFUNGO

Image
SALIM HAMAD,PEMBA KOCHA Mkuu wa timu ya Chipukizi Mwalim Mzee Ali Abdalla amezitaka timu zinazoshiriki ligi draraja la kwanza kanada ya Pemba,kujiandaa kiushindani ili kuhakikisha zinafanya vizuri katika mzunguko wa pili baada ya kupisha mfungo wa mwezi wa  ramadhani. Akizingumza na Mwanaspoti Kocha huyo alisema katika michezo yote 12 ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa timu nyingi  zilionesha dhahiri kwamba hazikuwa na maandalizi ya kutosha hivyo zinahitaji kujipanga vizuri na kukuzakuitia ladha ligi hiyo. Alisema ukiangalia kwenye matokeo timu nyingi zilikuwa zinatoka sare kiasi ya kwamba timu zinafanana kimatokeo ambapo alidai kuwa hicho ni kiashiria tosha kuonesha kwamba timu hazikuwa na maandalizi mazuri. ‘’Nidhahiri kwamba katika mzunguko ulimalizika timu nyingi hazikuwa na maandalizi ya kutosha zilishiriki tu kwani zilikuwa kila siku zinapokea taarifa ligi inaanza lakini haifanyiki jambo hilo limeziathiri sana klabu za Pemba ‘’alisema Mwalimu huyo. Alisema inagawa baadhi ya timu z

VILABU VYA DARAJA LA KWANZA KANDA YA PEMBA YATAKIWA KUJIPANGA KIMASHINDANI

  SALIM HAMAD,PEMBA KOCHA Mkuu wa timu ya Chipukizi Mwalim Mzee Ali Abdalla amezitaka timu zinazoshiriki ligi draraja la kwanza kanada ya Pemba,kujiandaa kiushindani ili kuhakikisha zinafanya vizuri katika mzunguko wa pili baada ya kupisha mfungo wa mwezi wa   ramadhani. Akizingumza na Mwanaspoti Kocha huyo alisema katika michezo yote 12 ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa timu nyingi   zilionesha dhahiri kwamba hazikuwa na maandalizi ya kutosha hivyo zinahitaji kujipanga vizuri na kukuzakuitia ladha ligi hiyo. Alisema ukiangalia kwenye matokeo timu nyingi zilikuwa zinatoka sare kiasi ya kwamba timu zinafanana kimatokeo ambapo alidai kuwa hicho ni kiashiria tosha kuonesha kwamba timu hazikuwa na maandalizi mazuri. ‘’Nidhahiri kwamba katika mzunguko ulimalizika timu nyingi hazikuwa na maandalizi ya kutosha zilishiriki tu kwani zilikuwa kila siku zinapokea taarifa ligi inaanza lakini haifanyiki jambo hilo limeziathiri sana klabu za Pemba ‘’alisema Mwalimu huyo. Alisema inagawa ba

VILABU VYA DARAJA LA KWANZA KANDA YA PEMBA VYATAKIWA KUJIPANGA KIMASHINDANI

  SALIM HAMAD,PEMBA KOCHA Mkuu wa timu ya Chipukizi Mwalim Mzee Ali Abdalla amezitaka timu zinazoshiriki ligi draraja la kwanza kanada ya Pemba,kujiandaa kiushindani ili kuhakikisha zinafanya vizuri katika mzunguko wa pili baada ya kupisha mfungo wa mwezi wa   ramadhani. Akizingumza na Mwanaspoti Kocha huyo alisema katika michezo yote 12 ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa timu nyingi   zilionesha dhahiri kwamba hazikuwa na maandalizi ya kutosha hivyo zinahitaji kujipanga vizuri na kukuzakuitia ladha ligi hiyo. Alisema ukiangalia kwenye matokeo timu nyingi zilikuwa zinatoka sare kiasi ya kwamba timu zinafanana kimatokeo ambapo alidai kuwa hicho ni kiashiria tosha kuonesha kwamba timu hazikuwa na maandalizi mazuri. ‘’Nidhahiri kwamba katika mzunguko ulimalizika timu nyingi hazikuwa na maandalizi ya kutosha zilishiriki tu kwani zilikuwa kila siku zinapokea taarifa ligi inaanza lakini haifanyiki jambo hilo limeziathiri sana klabu za Pemba ‘’alisema Mwalimu huyo. Alisema inagawa ba

MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA WAWI CHAKE CHAKE PEMBA WAMEDHAMIRIA KINGARISHA SEKTA YA MICHEZO

Image
SALIM HAMAD,PEMBA MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Bakari Hamad Bakari pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Khamisi Kassim Ali wamesema watahakikisha wanaiboresha sekta ya michezo kwa kutengeneza miundombinu ya Viwanja ambayo imekuwa kero kwenye Jimbo hilo. Wakizungumza na wananmichezo katika hafla ya kukabidhi jezi kwa timu mbali mbali za jimbo hilo Kisiwani hapa wamesema wanafahamu mazingira ya Viwanja hususani katika kipindi cha masika mvua zinapo nyesha. Mwakishi huyo Bakari Hamad Bakari alisema wanafahamu changamoto za viwanja ambapo timu nyingi za jimbo hilo zimekuwa na viwanja ambavyo sirafiki hasa zinaponyesha mvua za masika viwanja wao hujaa maji na kusababisha kushindwa kufanya mazoezi. Alisema mkakati wao ni kutengeneza Viwanja vitatu na kuvifanya kuwa vya kisasa ili timu za jimbo hilo ziweze kucheza katika mazingira mazuri kama timu nyengine za Tanzania bara. Alisema tayari waliashaanza kutengeneza kiwanja Cha Ndugu kitu kinachotumiwa na timu Machomane United na sasa wataendelea kuten

MBUNGE NA MWAKILISHI WA JIMBO LA WAWI WADHAMIRIA KINGARISHA SEKTA YA MICHEZO

Image
  SALIM HAMAD,PEMBA MWAKILISHI wa Jimbo la Wawi Bakari Hamad Bakari pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Khamisi Kassim Ali wamesema watahakikisha wanaiboresha sekta ya michezo kwa kutengeneza miundombinu ya Viwanja ambayo imekuwa kero kwenye Jimbo hilo. Wakizungumza na wananmichezo katika hafla ya kukabidhi jezi kwa timu mbali mbali za jimbo hilo Kisiwani hapa wamesema wanafahamu mazingira ya Viwanja hususani katika kipindi cha masika mvua zinapo nyesha. Mwakishi huyo Bakari Hamad Bakari alisema wanafahamu changamoto za viwanja ambapo timu nyingi za jimbo hilo zimekuwa na viwanja ambavyo sirafiki hasa zinaponyesha mvua za masika viwanja wao hujaa maji na kusababisha kushindwa kufanya mazoezi. Alisema mkakati wao ni kutengeneza Viwanja vitatu na kuvifanya kuwa vya kisasa ili timu za jimbo hilo ziweze kucheza katika mazingira mazuri kama timu nyengine za Tanzania bara. Alisema tayari waliashaanza kutengeneza kiwanja Cha Ndugu kitu kinachotumiwa na timu Machomane United na sasa watae

BINTI WA MIAKA 15 AMBAE NI MWANAFUNZI WA DARASA LA TANO APEWA UJAUZITO KWA MARA YA PILI NA SHEMEJI YAKE PEMBA.

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA. 12/4/2021.  Mtoto wa miaka 15  apewa ujauzito  kwa mara ya pili huko Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba Waswahili husema mchovya asali hachovi mara moja. Ni hakika hii ndio kawaida kwani asali ladha yake ni tamu na kama utaendekeza kuchovya basi huenda ukamaliza kibuyu. Mimi kwa hapa naulinganisha msemo huu na wale wanopenda kupata mazuri kwa njia ya mkato bila kujali athari zinazoweza kujitokeza, kwani akifanya mara ya kwanza akifanikiwa bila kupata tatizo lolote basi kwake hujenga mazowea na akaendeleza tabia yake bila kujali kwamba atajiharibia au kumuharibia anaemfanyia uovu hule. Na haya ndo aloyafanya kijana Mosi Othman Mosi mkaazi wa Muambe Wilaya ya Mkoani huko Kisiwani Pemba. Kijana huyu bila huruma wala kujali athari za anaemfanyia amediriki kwa mara mbili mfululizo kumpa ujauzito mtoto wa miaka 15 mbaye kwa sasa yupo darasa la tano. Alianza kumfanyia unyama huu akiwa darasa la nne ambapo kwa wakati huo alikuwa ana umri wa miaka kama 13

TAMWA INAENDELEA KUWAPIKA WANAJAMII JUU YA UTHUBUTU WA KUSIMAMA MAHAKAMANI KUTOA USHAHIDI.

Image
 NA FATMAN HAMAD PEMBA. Jamii imetakiwa   kusimama   kidete mahakamani kutoa ushahidi katika kesi za udhalilishaji ili   kuhakikisha watuhumiwa wa makosa hayo wametiwa hatiani na kupata adhabu. Akizungumza na wananchi wa Chokocho wilaya ya Mkoani Pemba katika mkutano wa uhamasishaji juu ya umuhimu wa kutoa ushahidi Ali Amour Makame kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka [ DPP]   Chake chake amesema kesi nyingi zinakwama mahakamani kutokana na kukosa ushahidi. Amesema   wengi wafanyaji wa matukio hao ni watu wa karibu na familia, hivyo wengi wanashindwa kwenda mahakamani kwa kuhofia ugomvi katika familia zao. ‘’Jamii   hawataki kutoa ushahidi wanaogopa watu wao   kufungwa   kwani wengi wanaofanya udhalilishaji ni watu wa karibu Ami, Baba wa kambo,   Mjomba na kadalika. Amesema Bila ya kupatikana ushahidi unaostahiki hakuwezi kuwa na kesi hivyo   ni   vyema jamii kuacha muhali   na waweko tayari kushirikiana na vyombo vya sheria ili kuwafichua wahalifu wanaowahujumu watoto na k

WADAU WA KUPINGA UDHALILISHAJI WAWAPIGA MSASA WANAOSULUHISHA KESI ZA UDHALILISHAJI MAJUMBANI KWAO.

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA  12/4/2021. Jamii imetakiwa kuondosha muhali na kuachatabia ya kufanya suluhu majumbani   kesi za udhalilishaji   jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa matendo hayo.   Akitoa elimu kwa wanafunzi na wazazi huko skuli ya Muambe wilaya ya mkoani   juu ya athari za utdalilishaji   msaidizi wa sheria   shehia ya mkanyageni   Haji Shoka   amewataka wanafunzi   pamoja na wazazi kuzipeleka katika vyombo vya sheria kesi za udhalilishaji. Amese licha ya elimu inayotolewa kwa jamii juu ya madhara ya   udhalilishaji   lakini bado kunabaadhi ya wazazi wanazifanyia suluhu majumbani kesi   hizo kwa kuhofia ugomvi katika familia zao hali ambayo inawakosesha haki   zao wahanga wa matendo hayo. ‘’Wazazi acheni ubishi kimbilieni kwenye vyombo vya sheria wakati unapotokea udhalilishaji’’ Alisema msaidizi wa sheria. Amesema   wakati umefika kwa Wazazi na Walezi kushirikiana na vyombo vya sheria juu ya kesi hizi za udhalilishaji ili kuondosha unyama huu ambao wanaendelea k

SERIKALI YATAKIWA KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA WALE WOTE WANAOZIFANYIA SULUHU KESI UDHALILISHAJI

Image
NA FATMA HAMAD PEMBA Serikali ya mapinduzi zanzibar imetakiwa kuwachukulia hatua kali za  kisheria  wale wote watakaobainika wanazifanyia suluhu majumbani kwao kesi za udhalilishaji kwa watoto. Hayo yamesemwa na wanafunzi wa skuli ya chokocho wilaya ya mkoani pemba katika mkutano wa kushajisha jamii juu ya umuhimu wa   kutoa  ushahidi mahakamani kwa kesi za udhalilishaji. Wamesema  bado wapo  wanafamilia  wanashindwa kwenda mahakamani kutoa ushahidi  na kuzifanyia suluhu wenyewe kwa wnyewe jambo ambalo linapelekea kuongezeka kwa udhalilishaji hapa nchini. ‘’tunaiomba serikali kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaoharibu ushahidi kwa makusudi. Kwa upande  wake  mwanafunzi  isha hassan ibrahim kutoka skuli ya sekondari  chokocho  amesema wakati umefika kwa wazazi na walezi kuwa mstari mbele kuzisimamia ipasavyo kesi hizo ili kuona wabakaji wanatiwa hatiani. Akitoa elimu kwa wanafunzi hao juu ya athari za utdalilishaji   msaidizi wa sheria   shehia ya mkanyageni shaban   ali   ame