TAMWA INAENDELEA KUWAPIKA WANAJAMII JUU YA UTHUBUTU WA KUSIMAMA MAHAKAMANI KUTOA USHAHIDI.
NA FATMAN HAMAD PEMBA.
Jamii
imetakiwa kusimama kidete mahakamani kutoa ushahidi katika kesi
za udhalilishaji ili kuhakikisha
watuhumiwa wa makosa hayo wametiwa hatiani na kupata adhabu.
Akizungumza
na wananchi wa Chokocho wilaya ya Mkoani Pemba katika mkutano wa uhamasishaji
juu ya umuhimu wa kutoa ushahidi Ali Amour Makame kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa
mashtaka [ DPP] Chake chake amesema kesi
nyingi zinakwama mahakamani kutokana na kukosa ushahidi.
Amesema wengi wafanyaji wa matukio hao ni watu wa
karibu na familia, hivyo wengi wanashindwa kwenda mahakamani kwa kuhofia ugomvi
katika familia zao.
‘’Jamii hawataki kutoa ushahidi wanaogopa watu
wao kufungwa kwani wengi wanaofanya udhalilishaji ni watu
wa karibu Ami, Baba wa kambo, Mjomba na
kadalika.
Amesema Bila
ya kupatikana ushahidi unaostahiki hakuwezi kuwa na kesi hivyo ni
vyema jamii kuacha muhali na
waweko tayari kushirikiana na vyombo vya sheria ili kuwafichua wahalifu
wanaowahujumu watoto na kuondokana na tatizo hilo.
Mapema Afisa Dawati la Jinsia kutoka wilaya ya Mkoani Rehema Mjawiei amesema kama jamii haitoacha muhali juu ya kesi hizi kutapelekea kuongezeka kwa udhalilishaji na kupatikana kwa watoto mabaradhuli.
‘’Hali ni
tete jamani ya udhalilishaji, acheni muhali ili tuweze kuwanusuru watoto
wetu,’’ Alisema Afisa dawati.
Hivyo
amewataka Wazazi na walezi kushirikiana kwa pamoja katika malezi na kufuatilia
nyendo za watoto wao ili kuwalinda na udhalilishaji.
Baadhi ya
wananchi waliohudhuria mkutano huo wamewataka
wahusika wa vyombo vya sheria wanaoshuhulikia kesi hizo kuziendesha kwa
uwadilifu wa hali ya juu na kutoa adhabu kubwa kwa watendaji wa makosa hayo
kwani kutasaidia kuondokana na matendo
hayo.
Mratibu wa chama cha wandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar [Tamwa] ofisi ya Pemba Fathiya Mussa Saidasema lengo la mkutano huo ni kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuripoti na kutoa ushahidi mahakamani pindi itakapotokezea udhalilishaji katika maeneo yao wanaoishi.
Comments
Post a Comment