Posts

Showing posts from September, 2020

Kamati ya Madili ya Baraza la Habari Tanzania-MCT-imesema ni marufuku kwa mujibu wa sheria ,Mandishi wa habari kuvaa sare za cha siasa .

  Kamati ya Madili ya Baraza la Habari Tanzania-MCT-imesema ni marufuku kwa mujibu wa sheria ,Mandishi wa habari kuvaa sare za chama cha siasa   wakati anapotekeleza majukumu yake hasa katika kipindi hichi cha kampeni za uchaguzi.   Hayo yamesemwa na Katibu mtendaji wa baraza la habari Tanzania Kajub  Mkajanga katika Mkutano wa Wandishi wa Habari na Vyanzo vya habari uliofanyika   katika ukumbi wa mikutano wa kiwanja wa michezo GombanChake chake Mkoa wa Kusini Pemba. Amesema sio jambo zuri kwa Mwandishi   wa habari kuvaa sare za chama kwani inaweza kuhatarisha usalama wake na vyombo vyake pamoja na kituo anachokifanyia kazi. ‘’Kwa mujibu wa sheria ya tume ya uchaguzi ni kosa kisheria mwandishi kuvaa sare ya chama, hili pia hata sisi MCT tunapiga marufuku hivyo hakikisheni mnajiepusha na vitewndo hivyo”alisisitiza. Aidha amesema mtu yoyote atakae mlazimisha   mwandishi   kuvaa nguo ya chama atakuwa amevunja Sheria   na kanuni za uandishi wa habari. Amefahamisha kuwa   wandishi