WADAU WAOMBA SHERIA ZINAZOHUSU MASUALA YA UDHALILISHAJI ZIFANYIWE MAREKEBISHO
NA FATMA HAMAD PEMBA. Mratibu wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Tamwa ofisi ya Pemba Fathiya Mussa Said amewataka wandishi wa habari kupaza sauti zao kwa kuzisemea sheria mbali mbali zenye mapungufu ambazo zinazohusu masuala ya udhalilishaji wa kijinsia ziweze kufanyiwa marekebisho ili zinaendana na hali ya sasa. Mratibu huyo ameyasema hayo huko ofisini kwake Mkanjuni Chake chake wakati akifunga mafunzo ya siku mbili yanayohusu mradi wa kuhamasisha hatua za kitaifa dhidi ya vitendo vya udhalilishaji Zanzibar kwa wandishi wa vyombo mbali mbali kisiwani Pemba . Amesema licha juhudi mbali mbali zinazochukuliwa ili kuondosha udhalilishaji lakini bado kuna vifungu vya sheria vinaleta ukakasi jambo ambalo linakwaza harakati za utetezi dhidi ya masuala hayo. ‘’Vipo vifungu mbali mbali vya sheria vinakandamiza masuala ya udhalilishaji hivyo ni jukumu lenu wandishi wa habari kuvipiga kelele ili kuona vinarekebishwa na