UONGOZI WA HALMASHAURI MICHEWENI WASHAURIWA.
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Spika wa
baraza la wawakilishi Zubeir Ali Maulid ameutaka uongozi wa halmashauri ya
wilaya ya Micheweni isiwatoleshe tozo kubwa wajasiriamali na wafanya biashara wadogo wadogo ambayo itakwamisha kuendeleza biashara yao.
Mheshimiwa Zubeir
ameyasema hayo wakati akifungua soko la wajasiriamali huko Tumbe wilaya
ya Micheweni Mkoa
wa Kaskazini Pemba.
Amesema
lengo la Serikali ni kuondoa kero za kuhama hama na kuainua kiuchumi
wajasiriamali hivyo basi watolesheni
tozo ngogo ambazo zinaendana na biashara zao jambo ambalo litawafanya
waendeleza biashara zao na kujipatia kipato cha halali.
‘’Niwaombe
nduzangu wa halmashauri wajasiriamali
wengi ni wanyonge hivyo msiwatoleshe kodi kubwa wafanya biashara wanaofanya
biashara zao katika soko hili ’’ alisema Mheshimiwa Zubeir.
Aidha
amewataka wafanya biashara na wajasiriamali kulitumia eneo hilo maalumu kwa ajili ya shuhuli zao za biashara kwani
kufanya hivyo kutasaidia kuipatia Serikali mapato.
Akitoa maelezo
ya Kitaalam juu ya mradi huo Katibu Mkuu Ofisi
ya Rais Tawala za mikoa, Serikali za mitaa na
Idara maalum za SMZ Issa Mahfudh Haji amesema mradi huo umegharimu jumla ya shilingi Bilioni
1 Milioni miatano thalathini na tatu Laki
tatu Arubaini na tatu mia tisa na thathini na tano.
Amesema
mradi huo utawanufaisha wajasiriamali mbali mbali wakiwemo wa biashara ya nguo,
Chakula na mboga mboga.
Comments
Post a Comment