Posts

Showing posts from September, 2023

JAMII YASHAURIWA KULEA WATOTO KATIKA MALEZI YA PAMOJA

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA   JAMII imetakiwa kushirikiana katika malezi ya pamoja ili kupatikana kwa kizazi chenye heshma na madili mema. Ushauri huo umetolewa na Kaimu Mratibu kutoka Ofisi ya mufti Pemba Said Khalfan Issa wakati akizunumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Chake chake amesema ni vyema jamii kurudisha Mila, Silka na tamaduni za kizanzibar katika kuwalea Vijana. Alisema zamani mtoto ilikuwa halelewi ni baba na mama pekee, bali kila mmoja alikuwa na nafasi yake, kama vile mwalimu wa madrasa, Shuleni na hata kwa wazazi wengine. ‘’Niombe jamii turudisheni tamaduni zetu za kuwalea watoto wetu katika malezi ya pamoja, ili waepukane na vitendo viou ikiwemo udhalilishaji pamoja na ukahaba,’’alisema. Alifahamisha kuwa sasahivi kumekuwa kukijitokeza viashiria vingi ambavyo ni hatari kwa watoto,hivyo wakati umefika kurudi katika misingi ya dini inavyoelekeza juu ya malezi,ili kulinda heshma ya wazanzibar. ‘’Kwa kweli hali imekuwa mbaya, kila mmoja hana amani juu

WANACHI WAHIMIZWA KUYATUNZA NA KUYAENZI MAZINGIRA YA BAHARI

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar,imesema itahakikisha   inachukua   hatua za makusudi za kudhibiti uharibifu wa mazingiara ya baharini  na kuwajengea uwelewa Wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira ya baharini. Hayo yamesemwa na Waziri wa Ujenzi mawasiliano na Uchukuzi Dokta Khalid Salim   Mohd   wakati akifunga maadhimisho  ya siku ya usafirishaji na usalama wa bahari  huko Gmbani Chake chake     Pemba. Alisema  binaadamu na viumbe baharini wanategemea bahari katika maisha yao ya kila siku hivyo ni wajibu wa wanachi kulipa umuhimu sualal la utunzaji wa mazingira ya bahari ili kulinda maisha ya viumbe wananchi baharini. Alisema  pamoja na umuhimu huo bado bahari inakabiliwa na changamoto kubwa ya uharibifu wa mazingira ikiwemo ukataji wa mikoko, utupaji taka ovyo baharini jambo ambalo husababaisha kupoteza maisha ya viumbe baharini pamoja na upandaji wa kina cha maji ya bahari. Alisema asilimia   70 ya wananchi wa Visiwa vya Zanzibar,wanategea

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA …………….. SIRI ya mtungi aijuaye kata……… Wahenga wametupa usia usemao ……Hasira hasara. Wakati mwengine hio hasira sio tu huathiri aliyefanya na aliyefanyiwa, bali watu wa karibu, mbali na hata jamii kwa ujumla. Hili linaonekana sana pale ndoa inapovunjika baada ya wana ndoa kuamua lipasuke tugawane mbao, lakini misumari ya hizo mbao huwachoma na kuwaumiza wengi, wakiwemo wana familia na hasa watoto. Mara nyingi pale wazazi wakiwa wametengana baada ya ndoa kuvunjika watoto hukosa huduma muhimu za maisha na kuathirika kimwili na kiakili na kiza hutanda katika safari yao ya maisha. Mwana harakati maarufu wa kulinda na kutetea haki za watoto kisiwani Pemba, Tatu Abdala Mselem, amekuwa mara kwa mara akiiomba jamii kuvunjika kwa ndoa isiwe sababu ya kila mzazi kufumbia macho wajibu wake wa malezi ya watoto. Hii ni kwa sababu mtoto  anapokosa huduma za lazima sio tu huwa mnyonge na kujiona kama yatima aliyekosa msaada, bali huwa hana furaha anapocheza, na akili yak

PACSO YATAKA ASASI ZA KIRAIA KUFANYA UTETEZI WA SERA, SHERIA ZINAZO MKANDAMIZA MWANAMKE.

Image
NA FATMA HAMAD,PEMBA ASASI za kirai zimetakiwa kuzisemea na kuzifanyia utetezi Sera na Sheria ambazo zina mkandamiza   mwanamke na mtoto wa kike wasifikie kwenye malengo yao, ikiwemo kwenye ngazi za mamuzi. Akiwasilisha mada mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka [Zalho] Pemba Siti Habibu Muhamed katika mkutano wa kuibua changamoto za kisera, sharia na kanuni zinazokwaza maendeleo ya wanawake kwa asasi za kutetea haki za wanawake huko Maktaba Chake chake Pemba. Mwanaharakati huyo alisema vipo vifungu kadhaa vya sharia vimekua vikimkandamiza mwanamke kushiriki katika sekta mbali mbali, hivyo ni vyema kusimama kidete kuleta ushawishi na utetezi, ili kuona zinafanyiwa marekebisho na mwanamke nayeye aweze kushika   nyadhifa za uongozi. ‘’Kama sisi ni wadau wa kutetea haki za wanawake, ni budi tushirikiane kwa kuzifanyia utetezi, ziweze kufanyiwa marekebisho ili kuhakikisha hazimkandamizi mwanamke na mtoto wa kike,’’ameeleza. Alisema miongoni mwa vifungu hivyo ni kifungu cha 67

WANANCHI WAKERWA NA MIUNDO MBINU MIBOVU HOSPITALINI

Image
NA FATMA HAMAD,PEMBA. WANANCHI   wa   kijiji cha Mtangani   wanaoishi   karibu   na   kituo   cha   afya   cha   Bagamoyo   wilaya ya Wete mkoa wa Kaskazini Pemba wanalalamikia   juu ya kukosekana kwa   eneo malumu   la kuchomea taka   za Hospitalini hapo, jambo ambalo linaweza kupelekea kutokea kwa maradhi hatarishi ya mripuko ikiwemo kuharisha.   Akizungumza na wandishi wa habari huko kijijini kwao   Nasra Ali Makame amesema kukosekana kwa eneo [shimo] malumu la kuchomea   taka katika kituo hicho kinawathiri, kwani wakati wa kuchomwa taka   moshi husambaa kwenye makaazi yao na kusababisha kukohoa na kupata   muamsho katika miili yao. ‘’Wanapochoma moto taka zao, moshi na harufu   yote inaingia humu ndani mwangu, Napata muwasho mimi na watoto wangu,’’alieleza.   Said Bakari Makame alisema kuwa watoto wote   wanachejeza karibu na shimo hilo, kwani hakuna uzio katika kituo hicho.   Alieleza kuwa kuna hatari kubwa ya waoto wanaoishi katika eneyo hilo kupata maradhi hatarishi ya

WAJAWAZITO WANAOJIFUNGULIA KITUO CHA AFYA WESHA, WALAZIMIKA KWENDA NA NDOO ZA MAJI WAKATI WA KUJIFUNGUA.

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA   KUKOSEKANA kwa huduma ya maji safi na salama, katika kituo cha Afya Wesha wilaya ya Chake chake, Pemba kunawalazimu wajawazito kujifungulia majumbani, jambo ambalo linahatarisha maisha ya mama na mtoto.   Wakizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo, wajawazito hao walisema wamekuwa wakipata shida hususani wakati wanapokwenda kujifungua, kwani hulazimika kwenda na ndoo zao za maji.   Walisema, wanategemea maji kutoka Mamlaka ya maji Zanzibar ‘ZAWA’ lakini ni zaidi ya miezi mitatu, hakuna huduma hiyo, hali inayopelekea usumbufu kwa wajawazito na kushindwa kujifungulia kituoni hapo.   Mmoja kati ya mama hao Asha Omar alisema wengi wao huona ni  bora tu wajifungulie majumbani, kwa kuhofia  kutokuwa na maji ya kujisafishia, baada ya kujifunguwa kwani kwa hali ya kawaida maji ya kwenye kidumu au ndoo kwa mzazi ni adhabu.   ‘’Tunapokwenda kujifunguwa waume zetu wanalazimika wabeba madumu ya maji, kupeleka hosptali na wala hayatutoshelezi, maana baada y

MTUHUMIWA WA KESI YA ULAWITI AOMBA AACHILIWE HURU

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA MTUHUMIWA wa kesi ya kunajisi mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 12, ambae ni mwenye ulemavu wa akili anaetambulika kwa jina la Khamis  Salum Ali mkaazi wa Selemu Wete [27], ameiomba mahakama ifute  kesi hiyo, kwani si ya ukeli ni ya uongo,[kusingiziwa]. Mtuhumiwa huyo ameiomba mahakama hiyo mbele ya hakimu wa Mahakama ya kupambana na makosa ya udhalilishaji iliyopo Wete mkoa wa kaskazini Pemba Ali Abdulrahman Ali alisema kuwa siku hiyo aliyosingiziwa kuwa amefanya tukio hilo hakuwepo maeneyo hayo, bali alikuwepo Chasasa kwenye shughuli zake za ujenzi. ‘ ’Mheshimiwa Hakimu mimi sjafanya tukio hilo hizo ni njama tu zilizopangwa na wazazi na wanakijiji wanibambikizie kesi ili ningie hatiani,’’alieleza. Alisema kuwa ushahidi uliotolewa na Madaktari pamoja na Askari wote ni wa uongo, hivyo ameiomba mahakama ifute kesi hiyo na imuachie huru, kwani hajafanya tukio hilo. Hakimu  Ali Abdul rahman Ali hakukubaliana na ombi la mtuhumiwa huyo, hivyo alimtaka arudi tena ruma

UZAZI WA MPANGO UNAVYOINUA WANAWAKE KIUCHUMI,

Image
  NA FATMA, HAMAD PEMBA KUPANGA kutamka au kufanya jambo kunasaidia kupata mafanikio mazuri au kupunguza hatari na athari za matatizo. Umuhimu huu wa kupanga pia unaonekana katika uzazi kwa vile uzazi wa mpango umethibitisha kuwa na faida nyingi kwa mama, mtoto, familia na taifa kwa jumla. Uislamu umeeleza wazi kuwa uzazi wa mpango sio unaplekea kuwa na afya njema ya mzazi na mtoto tu, bali pia furaha, amani na mapenzi katika familia. Baadhi ya watu  katika jamii  wamekuwa na imani potofu kwamba,  uzazi  wa mpango unapunguza kizazi na kusababisha   matatizo  kama  vile  kansa na   kutokwa  na damu nyingi  wakati wa hedhi.  Hili halina ukweli kwa sababu utafiti na ushuhuda wa wanawake waliojiunga na mpango huu unathibitisha kwamba hio ni dhana isiyokuwa na mshiko.  Asha Khamis wa Micheweni, Pemba,  anafurahia uamuzi wake wa kujiunga na auzazi wa mpango na kueleza kwamba ulimsaidi kupata muda wa kulea vyema watoto na kufanya biashara yake ya kuuza uji na mandazi. ‘’Nilikuwa