JAMII YASHAURIWA KULEA WATOTO KATIKA MALEZI YA PAMOJA
NA FATMA HAMAD, PEMBA
JAMII imetakiwa kushirikiana katika malezi ya pamoja ili kupatikana kwa kizazi chenye heshma na madili mema.
Ushauri huo
umetolewa na Kaimu Mratibu kutoka Ofisi ya mufti Pemba Said Khalfan Issa wakati
akizunumza na mwandishi wa habari hizi huko ofisini kwake Chake chake amesema
ni vyema jamii kurudisha Mila, Silka na tamaduni za kizanzibar katika kuwalea
Vijana.
Alisema zamani
mtoto ilikuwa halelewi ni baba na mama pekee, bali kila mmoja alikuwa na nafasi
yake, kama vile mwalimu wa madrasa, Shuleni na hata kwa wazazi wengine.
‘’Niombe
jamii turudisheni tamaduni zetu za kuwalea watoto wetu katika malezi ya pamoja,
ili waepukane na vitendo viou ikiwemo udhalilishaji pamoja na
ukahaba,’’alisema.
Alifahamisha
kuwa sasahivi kumekuwa kukijitokeza viashiria vingi ambavyo ni hatari kwa
watoto,hivyo wakati umefika kurudi katika misingi ya dini inavyoelekeza juu ya
malezi,ili kulinda heshma ya wazanzibar.
‘’Kwa kweli
hali imekuwa mbaya, kila mmoja hana amani juu ya mtoto wake, hajui ataishi vipi
mpaka afike kujielewa, turudini kwenye tamaduni zetu jamani tusiwape uhuru wa
kupitiliza vijana wetu,’’alifahamisha.
Asha Omar na
Said Juma wananchi kutoka Micheweni walisema kutokuwepo kwa malezi ya pamoja
yamechangia kwa kiasi kikubwa suala la mmon’gonyoka wa madili katika jamii.
‘’Zamani
mtoto akionekana anafanya kitendo kibaya anakamatwa na kuhukumiwa hapo hapo
bila ya kufikishwa kwa wazazi wake, hiyo ilikuwa ikiwafanya watoto kuishi kwa
woga, heshma na tabia njema,’’walifahamisha.
Nae mwanaharakati kutoka chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar [TAMWA] Pemba Fathiya Mussa Said alisema udhalilishaji bado ni tatizo linaloikumba jamii, hivyo ni vyema jamii kushirikiana katika malezi ili kuwalinda na janga hilo.
Comments
Post a Comment