WANDISHI WA HABARI PEMBA WAPIGWA MSASA
NA FATMA HAMAD Wandishi wa habari wametakiwa kuielimisha jamii kufahamu masuala ya Afya ya uzazi, ili kufahamu afya zao, na kuweza kupata tiba sahihi, jambo ambalo litasaidia kupunguza vifo vya mama na mtoto. Ushauri huo umetolewa na afisa mradi wa afya ya uzazi, wakati akielezea kuhusu mradi huo wa uzazi salama Zaina Abdala Mzee kwenye mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wandishi wa habari, kuandika habari zinazo husu masuala ya afya ya uzazi, yaliofanyika katika ukumbi wa Tamwa Chake Chake Pemba. Alisema kwa mujibu wa tafiti kutoka wizara ya afya, vifo vya mama na mtoto bado ni changamoto inayoikumba Jamii. Alisema wandishi wa habari wana nafasi kubwa katika jamii, hivyo ni vyema kuwandika habari pamoja na makala ambazo zitaisaidia jamii kufahamu masuala ya afya ya uzazi ili waweze kufika vituo vya afya kufanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu. ‘’Nyinyi waandishi wa habari mnaaminika zaidi katika jamii, hivyo ni vyema mkay