AACHIWA HURU BAADA YA KUDAIWA KUMUINGILIA KINYUME NA MAUMBILE MKE WAKE WA NDOA
NA FATMA HAMAD, PEMBA
MTUHUMIWA aliekuwa akidaiwa kumuigilia kinyume na maumbile mke wake, ameishangaza Mahkama maalum ya
kupambana na udhalilishaji ya mkoa kaskazini Pemba, kwa kudai kupatiwa ulinzi
baada ya kuachiliwa huru mahakamani hapo.
Baada ya kuachiwa huru mtuhumiwa huyo Mahakamani hapo aliomba Mahakama impatie
ulinzi ili apelekwe nyumbani kwao kutokana na hofu aliokua nayo kitu ambacho
mahakama ilikataa kufanya hivyo.
Mtuhumiwa huyo Haji Hamad Juma miaka 28, mkaazi wa Majenzi,
wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba aliishukuru mahakama hiyo kwa kutenda haki kwani hajafanya kosa hilo
bali alisingiziwa tu na mke wake kwa vile walikuwa hawana maelewano sikunyingi na
huku akimdai talaka.
‘’Naishukuru
mahakama kwa kuliona hilo, kwani sijamfanyia mimi mke wangu kitendo hicho,
ila naamini alinibambikizia tu kesi kwa
vile si kutaka kumpa talaka kama alivyokua akinidai kwa muda mrefu,’’ alieleza
mtuhumiwa.
Awali
Hakimu wa mahakama hiyo Ali Abdul Rahman
Ali alisema mtuhumiwa huyo amelazimika kumuachia huru, kutokana na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo kutomunganisha na kesi husika.
‘’Baada ya utetezi huo alioutoa yeye mshitakiwa kuwa sikunyingi mke wake akimdai
talaka na hakutaka kumpa, Mahakama imejiridhisha na kuona kwamba
hiyo ni kesi tu ya kusingiziwa na mke wake,’’ alisema hakimu huyo.
Mwendesha
mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP Juma Mussa Omar
aliambia Mahakama hiyo kuwa hakuridhishwa na uwamuzi huo na kuweka indhari ya
kukata rufaa.
‘’Mheshimiwa
hakimu
kwa uwamuzi uliofikiwa mahakamani hapa Ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka
haikuridhika na itakata rufaa juu ya shauri hilo,’’ alieleza.
Awali
ilidaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo alimuingilia kinyume na maumbile
mke wake wa ndoa, tokeo lililotokea machi 2 mwaka huu ambapo kufanya hivyo ni kosa
kinyume na kifungu cha 113 [a] sheria ya adhabu sheria namba 6/ya mwaka 2018
sheria ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment