Posts

Showing posts from February, 2022

WANANCHI WAHIMIZWA KUCHUKUA TAHADHARI JUU YA KUJIKINGA NA UGONJWA WA UKO19

  NA FATMA HAMAD PEMBA AFISA Mdhamini wizara ya Afya, ustawi wa jamii, wazee, jinsia na watoto Pemba Yakoub Mohamed Shoka, amewataka waandishi wa habari kuelimisha jamii kwa kutilia mkazo suala la unawaji wa mikono ndani ya jamii zao zilizowazunguka. Alisema, hivi sasa takwimu za kidunia zinasema kati ya nchi 60 zenye maambukizi ya Corona katika kiwango kikubwa kila watu wawili kati ya watatu kwenye watu Bilioni 1 ambao wameshapata maambukizi wamekosa huduma safi ya mikono majumbani mwao kwa kunawa maji tiririka na sabuni.   Akisoma hotuba kwa niaba ya Afisa mdhamini huyo Afisa uwezeshaji kinga na elimu ya afya Pemba Khamis Bilali Ali alisema, matumizi ya maji yamehimizwa na kutajwa hata katika vitabu vya dini hivyo aliitaka jamii kujenga utamaduni wa kunawa mikono ili kuepuka maradhi yanayoambukizwa. Aliyasema hayo katika mkutano uliowashirikisha waandishi wa habari ikiwa ni katika kuelekea maadhimisho ya siku ya unawaji mikono Zanzibar uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Archipil