Posts

Showing posts from March, 2022

VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIMAENDELEO.

Image
NA FATMA HAMAD PEMBA. ZAID ya Shilingi milioni miamoja zimetengwa na taasisi ya   SOS Zanzi bar kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao ni wajasiriamali ili waweze kujikwamua kimaisha na kutimiza ndoto zao kupitia biashara ndogo ndogo. Meneja miradi wa Shirika la SOS Kisiwani Pemba Abdalla Omar, amesema taasisi hiyo imetenga kiasi hicho cha fedha ili kuwasadia vijana katika nyanja tofauti ikiwemo Uvuvi. Biashara na Kilimo hasa katika kuelekeza nguvu katika uchumi wa Bluu. ‘’Tunataka kuwawezesha vijana ili weweze kujiajiri wenyewe jambo ambalo litawaepusha kujiingiza katika vikundi viovu’’ alisema meneja Abdala. Aidha alieleza kuwa   fedha hizo zitawasaidia vijana kufanya miradi mbali mbali ya kimaendeleo   ambayo itawapatia kipato kitakachowasaidia katika   familia   zao. Hivyo meneja huyo amewataka vijana kuchangamkia fursa hizo   za kimaendeleo ili waweze kuondokana na   umaskini uliokithiri. BaadhiyawadaukatikaKikaohichowalishauriserikalikufuatiliailimiradiyakuwawezeshavij

wandishi wa habari watakiwa kuepuka kuandika habari zinazo wadhalilisha watu wenye ulemavu

  NA FATMA HAMAD PEMBA 9/3/ 2022. Wandishiwa habari wametakiwa kufuata miko na madili ya kazi yao wakati wanapoandika   na kuripoti habari za watu wenye ulemavu ili kulinda utu, heshima ya kundi la watu hao. Akizungumza   katika mkutano wa kuwajengea uwezo wa kuripoti habari za watu wenye ulemavu   wandishi wa habari wa Unguja na Pemba huko hoteli ya Maru maru Juma Salum Ali kutoka    Shujuwaza amesema watu wenye ulemavu wanahaki ya kulindwa, kuheshimiwa na kuthaminiwa kama   watu wengine. ‘’Niwaombe   sana   epukeni kutumia majina mabaya wakati mnapoandika na kuripoti habari za watu wenye ulemavu   ambayo yanaleta viashiria vya udhalilishaji kwa watu wenye ulemavu’’ alisema Juma Salum. Kwa upande wake Ussi Khamis   ameeleza kuwa watu wenye ulemavu bado wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo Ajira Elimu na kushika nafasi za uongozi, hivyo   ni vyema wanahabari kupaza sauti zenu   kuzisemea kero hizo hali ambayo itasaidia kuondosha matatizo hayo.

wandishi wa habari wahimizwa kuandika habari za watu wenye ulemavu

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA       8 /3/ 2022. Wandishi   wa   habari   wametakiwa   kujikita zaid maeneo ya   Vijijini ili kuibua kero na changamoto ambazo zimekuwa zikiwakumba watu wenye ulemavu. Wito huo umetolewa na Waziri wanchi ofisi ya makamo wa kwanza wa rais Zanzibar Saada Mkuya Salim wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wandishi wa   habari wa   vyombo mbali mbali   Zanzibar   huko ukumbe wa Maru maru Hoteli kisiwani unguja. Alisema   watu wenyeulemavu wamekuwa wakikumbana na matatizo mbali mbali hivyo ni wakati wandishi kujitoa na kuzibua   kero ili ziweze kufikia kwa jamii na kupatiwa ufumbuzi. ‘’Nyinyi wandishi wa habari   mnamchango mkubwa wa kubadilisha maisha ya watu wenye ulemavu hivyo msikae tu bali nendeni mkaibuwe   na muweze kuyatoa katika vyombo vya habari jambo ambalo litamfanya kila aneguswa na hilo aweze kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa nafasi yake alionayo’’ alieleza waziri. Kwa upande mwengine waziri sada aliwasihi wazazi ambao wana watoto wenye