VIJANA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIMAENDELEO.






NA FATMA HAMAD PEMBA.

ZAID ya Shilingi milioni miamoja zimetengwa na taasisi ya  SOS Zanzi bar kwa ajili ya kuwawezesha vijana ambao ni wajasiriamali ili waweze kujikwamua kimaisha na kutimiza ndoto zao kupitia biashara ndogo ndogo.

Meneja miradi wa Shirika la SOS Kisiwani Pemba Abdalla Omar, amesema taasisi hiyo imetenga kiasi hicho cha fedha ili kuwasadia vijana katika nyanja tofauti ikiwemo Uvuvi. Biashara na Kilimo hasa katika kuelekeza nguvu katika uchumi wa Bluu.

‘’Tunataka kuwawezesha vijana ili weweze kujiajiri wenyewe jambo ambalo litawaepusha kujiingiza katika vikundi viovu’’ alisema meneja Abdala.

Aidha alieleza kuwa  fedha hizo zitawasaidia vijana kufanya miradi mbali mbali ya kimaendeleo  ambayo itawapatia kipato kitakachowasaidia katika  familia  zao.

Hivyo meneja huyo amewataka vijana kuchangamkia fursa hizo  za kimaendeleo ili waweze kuondokana na  umaskini uliokithiri.

BaadhiyawadaukatikaKikaohichowalishauriserikalikufuatiliailimiradiyakuwawezeshavijanapamojanakuwapatiataalumasahihiyauendeshajinausimamiziwamiradi.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.