WANDISHI WA HABARI WAPEWA MBINU.
FATMA HAMAD PEMBA. Wandishi wa habari Nchini wamekumbushwa kuitumia mitandao ya kijamii kwa kuandika habari zenye ukweli na zenye ubora ili kuepuka kuingia katika migoghoro isio ya lazima. Ukumbusho huo umetolewa na Mwenyekiti wa Jumuia ya wandishi wa habari Pemba Pres Clab [PPC] Bakar Mussa Juma wakati akizungumza na wandishi wa habari wa mitandao katika mafunzo juu ya ulinzi na usalama wa mitandao ya kijamii huko ofisi ya Ppc Chake chake Pemba. Amesema mitandao ya kijamii ndio chombo kinachofikisha ujumbe haraka kwa jamii hivyo ni vyema kuwa makini wakati wanaporusha habari zao ili iweze kuwajenga na kuwa huru katika kazi zenu. Amesema vyombo vya habari ndio sauti ya wasio na sauti hivyo sasa ni wakati wa Wandishi kubadilika na waweze kuandika habari zenye uhakika ambazo zitaleta tija kwa Jamii. ‘’Mitandao ya kijamii ndio chombo kinachofikisha ujumbe kwa haraka katika jamii hivyo lazima muwe makini sana katika kutumia hii mitandao kwani kumekua na wat