NA FATMA HAMAD PEMBA.
Mtuhumiwa wa kesi ya
ulawiti Nuhu Kombo Nuhu ameiambia mahakama
ya mkoa inayoshuhulikia kesi
za udhalilishaji iliyopo mkoa wa
Kaskazini Pemba kumpa ruhusa kwenda kutafuta mashahidi ili waweze kuja kutoa
ushahidi.
‘’Mheshimiwa hakimu
mimi nimo ndani nitawapata vipi hao mashahidi naomba niruhusu nitoke
nikawatafute’’ alisema mtuhumiwa.
Hakimu wa mahakama
hiyo Ali Abdulrahman Ali alimtaka mtuhumiwa huyo kutaja majina ya
mashahidi waweze kupelekewa barua ya
wito ili waweze kufika mahakamani na kutoa ushahidi.
‘’Wewe upo rumande
hatuwezi kukuruhusu kwenda kutafuta mashahidi kama umeshindwa sema tufunge
ushahidi’’ alisema hakimu.
Hivyo utaendelea
kubaki rumande hadi tarehe 24/10/2022 kwa ajili ya kuendelea na hatua ya
utetezi.
Tukio hilo lilitokea tarehe 13/ 12/
2021 majira ya sa moja asubuhi huko kijichame wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo mtuhumiwa alimlawiti
kijana mwenye ulemavu wa akili.
Ilidaiwa kuwa kufanya hivyo ni
kosa kinyume na kifungu cha 116[1] cha
sheria nambari 6/2018 sheria ya
Zanzibar.
Comments
Post a Comment