Ni ipi nafasi ya familia katika kuwashajiisha watoto wa kike kushiriki michezo.
Na, Fatma Hamad NA FATMA HAMAD, PEMBA Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, kupitia idara yake ya michezo, imekuwa ikitoa fursa mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo ajira, kushiriki mabonanza nje ya Zanzibar. Hilo limekuja kwa wazazi kutokuwapa nafasi watoto wa kike kushiriki michezo, kwani bado wanahisi kwa mwanamke ni uhuni na kupelekea siku zote kubaki nyuma kimichezo. Licha ya Serikali kutoa fursa nyingi za kimaendeleo, bado ushiriki wa wanawake na watoto wa kike, ni mdogo ukilinganisha na wanaume hapa visiwani Zanzibar, hususan kisiwa cha Pemba. Wazazi na walezi wanayo kila sababu ya kuhakikisha wanawapa nafasi (fursa) watoto wa kike, kushiriki kwenye michezo ili kuona nawao wanajinyakulia fursa zilizomo kwenye Sekta ya michezo. Kwani wapo wengi wamekuwa ni wachezaji wazuri wakati wanapokuwepo skuli, wanapomaliza vipaji hivyo hupotea. Makala hii itangazia nafasi ya wanajamii (familia ) katika kuwashajiisha watoto wa kike, kushiriki ipasavyo kwenye michezo. WATOTO Mtoto F...