Ni ipi nafasi ya familia katika kuwashajiisha watoto wa kike kushiriki michezo.
Na, Fatma Hamad
NA
FATMA HAMAD, PEMBA
Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar, kupitia idara yake ya michezo, imekuwa ikitoa fursa
mbali mbali za kimaendeleo ikiwemo ajira, kushiriki mabonanza nje ya Zanzibar.
Hilo
limekuja kwa wazazi kutokuwapa nafasi watoto wa kike kushiriki michezo, kwani
bado wanahisi kwa mwanamke ni uhuni na kupelekea siku zote kubaki nyuma
kimichezo.
Licha
ya Serikali kutoa fursa nyingi za kimaendeleo, bado ushiriki wa wanawake na
watoto wa kike, ni mdogo ukilinganisha na wanaume hapa visiwani Zanzibar,
hususan kisiwa cha Pemba.
Wazazi
na walezi wanayo kila sababu ya kuhakikisha wanawapa nafasi (fursa) watoto wa
kike, kushiriki kwenye michezo ili kuona nawao wanajinyakulia fursa zilizomo
kwenye Sekta ya michezo.
Kwani
wapo wengi wamekuwa ni wachezaji wazuri wakati wanapokuwepo skuli, wanapomaliza
vipaji hivyo hupotea.
Makala
hii itangazia nafasi ya wanajamii (familia ) katika kuwashajiisha watoto wa kike,
kushiriki ipasavyo kwenye michezo.
WATOTO
Mtoto
Fatma Mkubwa mwenye umri wa miaka 15 mkaazi wa Mkoani anasema, wazazi
wawaruhusu watoto wa kike kushiriki michezo, kwani nawao wanatamani kufika
mbali.
‘’Nasisi
watoto wa kike tunauwezo wa kucheza na tukaweza kufanya vizuri, hivyo wazazi
musituzuie na tunataka kukuza vipaji vyetu,’’anasema.
Anasema
anacheza mpira wa mikono katika timu ya watoto wenye ulemavu na ndoto yake siku
moja ni kuona amefika nchi za Ulaya, kwa ajili ya michezo.
Aisha
Ali mwenye umri wa mika 17 mkazi wa Sizini anasema, anapenda riadha pamoja na mpira
wa miguu, ingawa aliishia kucheza tangu akiwa anasoma, familia yake haimruhusu tena kwani anaonekana akiendelea
atahunika.
‘’Natamani
siku moja nije niwe mwanamichezo marufu duniani, ila kipaji changu kinadumaa si
kupata kuendelezwa,’’anasema.
JAMII.
Kulthum
Faki wa Konde, anasema wazazi wawaruhusu watoto wao wa kike kujiunga kwenye
michezo kwani, michezo ni moja njia inayopelekea kujipatia ajira.
‘Tumekua
tukishuhudia vijana wengi wakipata ajira kama vile vikosi, hivyo wazazi
msiwazuie watoto wa kike kujiunga na michezo, na wao wanayo haki ya kupata hizo
ajira,’’anaeleza.
Khatib
Iddi Mwalimu mkazi wa Mkoroshoni Chake chake, anasema michezo huimarisha afya,
hivyo ni vyema wazazi kutoa fursa kwa watoto wao wa kike kujiunga
na michezo, ili kuwakinga na maradhi na kuwa wakakamavu ambapo itawasaidia
kufanya vizuri kwenye masomo yao.
‘’Wazazi
wapeni nafasi watoto wa kike wajiunga kwenye michezo, kwani kutawasaidia kuwa
na afya njema,’’anaeleza.
Juma
Kombo Hija mkaazi wa Chamboni Micheweni amewataka wazazi na walezi kuwa na
hamasa ya kuwashajiisha watoto wa kike kushiriki kwenye michezo ili, nawao
wajione kama ni sehemu ya jamii ambayo inahitaji kupata maendeleo.
VIONGOZI
WA SERIKALI
Afisa
Mdhamini wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mfamau Lali Mfamau
anasema, bado wananchi hususani Pemba, hawajakuwa na mwamko juu ya la michezo
kwa mtoto wa kike, kwani wanahisi ni kitendo kinachokwenda kinyume na madili.
‘’Tukiangalia
vipaji tunavyo mitaani vya michezo kwa watoto wa kike, ila wazazi hawawaruhusu,’’anaeleza.
Anasema
idara ya michezo imekuwa ikitoa fursa nyingi kupitia michezo, hivyo ni wakati
kwa wanajamii kuwamka na kuwashirikisha watoto wao wa kike kwenye michezo, ili
nawao wafaidike na fursa hizo.
Khamis
Hamad Juma Naibu Katibu mkuu wa Shirikisho la mpira wa Miguu Zanzibar (ZFF) Ofisi
ya Pemba, anasema ipo haja kwa serikali, pamoja na wadau wa michezo,
kuwaelimisha wazazi juu ya umuhimu wa
michezo.
Ansema
ili wawaruhusu watoto wao wa kike kwenye
michezo, kwani siku moja inaweza kuja kuwa mkombozi wa maisha yao.
WANAHARAKATI
Fat
-hiya Mussa Said anasema bado wazazi wanahitaji kupewa elimu, ili waweze
kufahamu umuhimu wa michezo kwa mtoto wa kike, waweze kuwaunga mkono.
Anasema
kutokana na itikadi potofu zinazojengeka kwa jamii, kwamba michezo kwa
mwanamke ni uhuni, wanashindwa kuwapa
nafasi watoto wao wenye vipaji vya michezo.
‘’Utakuta
watoto wa kike wengi wanaishia kucheza michezo wakiwa skuli tu, wakimaliza
vipaji hivyo hufa, kwa sababu imejengeka michezo ni kwa wanaume tu,’’anaeleza.
Katiba
ya Zanzibar ya mwaka 1984 kifungu cha 12 (1) kinafafanua kuwa, watu wote ni
sawa mbele ya sheria, na wanayo haki bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata
haki sawa.

Comments
Post a Comment