Posts

Showing posts from January, 2024

JAJI MKUU ZANZIBAR ATAKA WANAFUNZI WA VYUO VYA MAFUNZO KUPATIWA ELIMU YA USHAURI NASAHA

Image
                                 NA FATMA HAMAD, PEMBA Mahikimu wa mahakama za kadhi, Makamanda wa Vyuo vya mafunzo kisiwani Pemba wametakiwa kushirikia na Idara ya Msaada wa kisheria   kuwapa   elimu   ya   ushauri   nasaha wanafunzi    wa   Vyuo   vya   mafunzo ili waweze kubadilika na kuwa na tabia njema. Agizo hilo limetolewa na   Jaji mkuu wa Zanzibar Ramadhan Khamis Abdala wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na Makamanda wa Vyuo vya mafunzo kisiwani Pemba. Alisema wengi wanaofikwa na mtihani wa kwenda kwenye   vyuo vya mafunzo wanahisi kama wameonewa, hivyo ni vyema kuanzishwa utaratibu wa kupewa ushauri nasaha ili waweze kuondokana na mawazo hayo,na kuona watakaporudi katika familia zao   wamebadilika tabia na kuwa Raia wema. ‘’Wenzetu hawa   wanapokuja humu vyuoni huwa wanathirika kisaikologia, na kuhisi Serikali imewaonea hivyo ni budi kuwapa Mawaidha pamoja na ushauri nasaha ili ziweze kurudi   akili zao, alisema. Aidha alisema ni vyema kupatiwa misada midogo mi

Wanawake wawaonesha wenzao njia kujitumbukiza kwenye siasa

Image
Changamoto, vikwazo, bezo kisha safari iendelee   NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR UONGOZI ni haki ya kila mtu, awe mwanaume au mwanamke. Tena hapa tunajifunza kuwa, hata kundi la watoto wa kike ama wakiume, wanaweza kuwa viongozi kwa aina yao na sehemu waliyo ndani ya jamii yao. Jamii imeshazowea kuona mwanaume ndio anaeweza kuwa kiongozi na kusimamia nchi katika hali zote, kuliko wanawake nahii kutokana na mitazamo yao isijengwa kimamtiki. Ingawa mtazamo huu, unaweza ukaondoka kwasababu mwanamke ameweza kuongoza familia na kuweza   kusimama imara,   kwahivyo hatoshindwa kuisimamia nchi nzima. Mfano hai na wa kweli kwa sasa ndani ya taifa la Tanzania, rais anayewaongoza wananchi wastani wa milioni 60 ni Dk. Samia Suluhu Hassan (mwanamke), na kila mmoja ni shahidi hajatetereka kwenye nafasi hiyo. Tena anasimamia vyema familia yake, pamoja na wananchi wake na kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea katika nchi na mengi yameongelewa kuhusu yeye bali hakukata tamaa. KWA NINI WAN

MAHAKIMU NA MAJAJI WAHIMIZWA UWADILIFU KWENNYE KUTOA HAKI

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA Watendaji wa Mahakama kisiwani Pemba wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu zaidi ili kuhakikisha Wananchi wote wanapata haki zao bila ubaguzi. Hayo yamesemwa na Mrajis wa mahakama Zanzibar Valentina Andrew Catema wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mahakama mkoa wa     wa Kaskazini Pemba. Amesema suala la utoaji wa haki ni kipengele muhimu katika uendeshaji wa kesi, hivyo wanadhima kubwa ya kuhakikisha wanafanya kazi bila ya ubaguzi jambo ambalo litasaidia wananchi kujenga imani na Mahakama. ‘’Niwambie ndugu zangu mnadhima kubwa kwa jamii, hivyo fanyeni kazi kwa umakini ili kuhakikisha mnatenda haki,alisema. Aidha aliwataka watendaji hao kudumisha umoja na mshikamano wao katika utendaji wa majukumu yao, kwani kufanya hivyo kutawawezesha kufanya kazi   kwa ufanisi wa hali ya juu.   Kwa upande wake hakimu dhamana wa Mahakama ya Mkoa Wete Mumin Ali Juma alisema licha ya mafanikio makubwa waliofikia lakini bado wanakabiliwa na changamoto ya uh

UCHUMI MDOGO ULIMFANYA MWANAMKE AWE KIONGOZI

Image
    NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR Binaadamu siku zote hutakiwa ajuwe alipo na wapi anataka kwenda. Katika maisha hii huwa ni ndoto ambayo humpelekea mtu kupitia mengi, baadhi yao yakiwa ni mtihani mmoja baada ya mwengine. Jambo muhimu ni kutokata tamaa na kuendelea kupambana na pale unapoteleza au kuanguka unapaswa kuinuka na kuendelea na safari huku ukiwa na matumaini ya siku moja utafika huko unapokusudia kwenda. Bi Huzaima   Ali Hamdani, miaka 51, ambae ni mjasiria mali wa uchoraji piko   na biashara ya vyakula, ni mmoja wa wanawake aliyekabiliana na mithani mingi katika safari yake ya uchoraji aliyoianza 1997. Kila alipokutana na kikwazo hakukata tamaa, bali aliendelea kupambanana na   kuanza biashara nyengine, ikiwemo ya kuuza urojo, maandazi na chapati, ili kuhakikisha anajipatia kipato cha halali cha kujiendesha kimaisha. "Kila siku asubuhi nauza urojo, mandazi chapati na juisi na ikifika jioni nauza supu ya utumbo na chapati,"alisema. Alipomsikia Rais wa