Wanawake wawaonesha wenzao njia kujitumbukiza kwenye siasa

Changamoto, vikwazo, bezo kisha safari iendelee

 NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR

UONGOZI ni haki ya kila mtu, awe mwanaume au mwanamke.

Tena hapa tunajifunza kuwa, hata kundi la watoto wa kike ama wakiume, wanaweza kuwa viongozi kwa aina yao na sehemu waliyo ndani ya jamii yao.

Jamii imeshazowea kuona mwanaume ndio anaeweza kuwa kiongozi na kusimamia nchi katika hali zote, kuliko wanawake nahii kutokana na mitazamo yao isijengwa kimamtiki.

Ingawa mtazamo huu, unaweza ukaondoka kwasababu mwanamke ameweza kuongoza familia na kuweza  kusimama imara,  kwahivyo hatoshindwa kuisimamia nchi nzima.

Mfano hai na wa kweli kwa sasa ndani ya taifa la Tanzania, rais anayewaongoza wananchi wastani wa milioni 60 ni Dk. Samia Suluhu Hassan (mwanamke), na kila mmoja ni shahidi hajatetereka kwenye nafasi hiyo.

Tena anasimamia vyema familia yake, pamoja na wananchi wake na kutatua changamoto mbalimbali zinazotokea katika nchi na mengi yameongelewa kuhusu yeye bali hakukata tamaa.

KWA NINI WANAWAKE HAWAONEKANA KWENYE SIASA?

Asiata Said Abdallah ambae ni mueka hazina wa Kanda ya Unguja katika Chama cha Demokrasia na Maeneleo CHADEMA,  anasema amejiunga katika siasa mwaka 1994 katika chama  hicho na kugombea katika nafasi ya vijana na hakubahatika kuipata.

"Nilipojiunga katika chama, nikaona nigombanie katika upande wa vijana, mkoa wa Kilimanjaro ila sikubahatika kupata,na sikukata tamaa nikaendelea kugombania tena mwaka mwingine pia sikubahatika kupata," anasema.

Anataja moja ya vikwazo vilivyopelekea kushindwa kwanza ni elimu ya kutosha kuhusiana na siasa,kutokuwa na mahusiano na vijana wengine pamoja na kutokuwa na uwezo wa kuwashawishi vijana.

"Mume wangu wa mwanzo alikuwa hapendi nijihusishe kwenye siasa,na baada ya muda ndoa kuvunjika, nilindeleza ndoto zangu na nikabahatika mume mwengine nashukuru ananipa nguvu katika kushirikisiasa,"anaeleza.

Anaona kwenye sisa zipo fursa mbali mbali, iwapo wanawake watatuliza akili zao, ikiwemo kujenga uhusiano na wananchi pamoja na kujipima kiuongozi kwa kule kugombea na wanaume mbali mbali.

" Miaka ya nyuma ilikuwa tunaona mwanamke wa kiislamu hawezi kusimama katika jamii kutokana na imani yetu, lakini sasa hivi viongozi wa dini nao wanatuelimisha,"anafafanua.

Sababu iliyopelekea kuingia kwenye siasa ni kurithi nyayo za mama yake  kwasababu yeye ni mwasisi wa chama cha chadema maulidah Anna komu

Aidha alisema miongoni mwa sambabu zinazopelekea wanawake kuwa kidogo katika siasa ikiwemo kutojiamini,woga,kutokuwa na moyo wa ujasiri, ambapo haya yalishajiengwa na wanaume tokea asili.

 Mgeni Ali Haji ambae amegombae nafsi ya uwakilishi wa viti maalumu nafasi za wasomi katika chama cha Mapinduzi CCM mwaka 2020, na kutobahatika kupata na kuelezezea sababu mbalimbali zilizopelekea kutopata fursa hiyo.

"Sababu iliyonifanya nikose kubwa ni kukosa matayarisho yangu binafsi, ikiwemo wapiga kura kutonielewa kwa undani pamoja na kukosa uwezo wa kufanya kampeni,’’anaeleza.

Lakini anaona wapiga kura wakati mwengine hawataki kubadili mgombea mwingina hata kama yule waliyenae hawajatekeleza ahadi zao ambazo aliwatangaazia wakati wa kampeni.

 Sambamba na hayo alisema sababu nyengine  kura hazikutosha kushinda nafasi hiyo na kubahatkika kupata kura 36 na mwezangu alipata kura zaidi ya 100.

 Aidha alisema hatua mbalimbali amechukua baada ya kushindwa, kuingia katika siasa ikiwemo kuzidi kujifunza katika masuala ya uongozi na kushiriki katika mambo ya kijamii.

"Kwavile jamii ndiyo husika katika uongozi, ndiyo wanaweza kukufahamu kwahiyo nimeona nifanye hivyo pia kuongeza elimu nalo kiupande changu ni jambo muhimu sana,’’anasema.

Licha ya yote hayo aliyopitia mpango wake wa badae, ni kuja kugombania tena uongozi na kupata matumaini ya kuja kushinda kwasababu ameshapata taaluma ya uwongozi.

Anaona kuwa, wanawake wanaopate fursa ya kugombea ni lazima wapewe elimu ya kutosha, kwanza kuyajua mazingira ya siasa, pili kuelimishwa kuwa unapoomba unaweza kupata au kukosa, ambapo ni sawa na asiyeomba ana hakika ya kukosa.

‘’Wapo wanawake wanadhani kama vile hawana haki ya kugombea, na wanaona kuna familia ama watu maaluma ndio wenye haki ya kugombea, jambo ambalo sio sahihi,’’anasema.

"Nasaha zangu kwa wanawake wanzangu waliopo madarakani  wawashajihishe wanawake wengine, ili nao waweze kugombania na kuondoa hofu, na waendelee kufanya vizuri katika majukumu yao kwasababu itawasaidia  kuwepo kwa  wigo kwa wanawake wegine,’’anasema.  

"Wanawake tukiwa wengi katika uongozi tutapata fursa ya kutoa mawazo na ushauri kuhusiana na maswali yanayowahusu wanawake na watoto na jamii kwa ujumla kina mama ni lazima tubadilike uongozi ni tunu gombea uongozi uwe mtetezi wa wanawake wengine,’’anaeleza. 

Mwakilishi wa Jimbo la Konde Pemba,Zawadi Amour Nassor, anasema ametumia njia mbalimbali yakuweza kutatua vikwanzo ambavyo amepitia kwa lengo la kuwa kiongozi.

"Kwanza sikukata tamaa, wakati nilipokuwa nagombania, maana kwa vile nilishawafuata walionitangulia, waliniambia ambayo yanawezakujitokeza katika safari yangu ya siasa,’’anasema.

Profesa Issa Haji Zidi, alifafanua kuwa dini ya kuislamu haijakataza kuwepo kwa kiongozi mwanamke isipokuwa mwanamke anatakiwa kufata taratibu na sheria za kiislamu.

Anaeleza kuwa katika enzi za Mtume Muhammad (S.A.W )mwanamke alikuwa kiongozi katika vita na mambo mengine tofauti na kote aliweza kufanikisha.

"Mwanamke wa mwanzo aliyeshika na kukubaliwa wadhifa wa ushauri kwa Mtume (SAW) alikuwa mama yetu mkubwa, Sayyidatuna Khadija binti Khuwayld (RA), ambaye alikuwa mshauri wake mkuu,’’anafafanua.

Hapa Mratibu  wa kuinua wanawake katika uongozi kutoka chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania  (TAMWA Zanzibar), Mariyam Ame, anasema wanatoa elimu mbalimbali, kwa wanawake ambao wanahitaji kuwa kiongozi, ili wajitambua na kutatua changamoto za kiuongozi.

"Nahii inawapa hamasa na kuweza kutambua haki zao za kidemokrasia, ikiwemo haki ya kupata elimu afya pamoja namiundombinu .

Maryam anasema hadi sasa zaidi ya wanawake 172 wamepatiwa mafunzo ya uwongozi kutoka Unguja na Pemba, pamoja na kutambua vikwazo na namna ya kukabiliana navyo.

Aidha aliwanasihi wanawake wanaotaka kuingia kwenye uongozi kutokuwa na hofu,kama Katiba inavyosema katika serikali zote mbili inavyoelezea pamoja na mikataba mbalimbali ya kitaifa na kikanda pamoja na kuwa karibu na chama chake.


 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.