Posts

Showing posts from May, 2021

SIGARA NA TUMBAKU HUSABABISHA MARADHI YA SARATANI YA SINGO YAKIZAZI, KENSA YA DAMU NA KISUKARI KWA WATUMIAJI WA VILEO HIVYO

Image
Wizara ya Afya Zanzibar imesema  utumiaji wa vileo vya Sigara na Tumbaku ni moja ya chanzo kinachopelekea kupata maradhi hatarishi kwa watumiaji wa vileo hivyo. Akizungumza na Wandishi wa habari mratibu wa kitengo cha Maradhi yasioambukiza Zanzibar Zuhura Saleh Amour katika mkutano   juu ya udhibiti wa matumizi ya Tumbaku huko ukumbi wa Makamo wa Pili wa Rais Chake chake Pemba. Amesema imebainika kuwa wengi watumiaji wa Sigara na Tumbaku hupata  maradhi ya Kisukari, Kensa,Ugonjwa wa akili na ugonjwa wa moyo. ‘’Tumbaku ni hatari jamani ukiitumia kwa kuvuta ama kwa kutafuna’’ alisema Bi Zuhura. Amesema kuwa shirika la Afya ulimwenguni limesema zaidi ya watu milioni 8 hufariki dunia kila mwaka ulimwenguni kutokana na matumizi ya tumbaku ambapo kati hao  milioni 7 wanaofariki ni wale wanaovuta ama wanaotafuna. Ameleza kuwa zaid ya watu Bilioni moja nukta tatu ya wathirika wa tumbaku ni kutoka katika Nchi zenye kipato cha chini. ‘’Sisi Nchi zetu ndio zaid watu wanathirika na matumizi ya tum