SIGARA NA TUMBAKU HUSABABISHA MARADHI YA SARATANI YA SINGO YAKIZAZI, KENSA YA DAMU NA KISUKARI KWA WATUMIAJI WA VILEO HIVYO


Wizara ya Afya Zanzibar imesema  utumiaji wa vileo vya Sigara na Tumbaku ni moja ya chanzo kinachopelekea kupata maradhi hatarishi kwa watumiaji wa vileo hivyo.
Akizungumza na Wandishi wa habari mratibu wa kitengo cha Maradhi yasioambukiza Zanzibar Zuhura Saleh Amour katika mkutano  juu ya udhibiti wa matumizi ya Tumbaku huko ukumbi wa Makamo wa Pili wa Rais Chake chake Pemba.

Amesema imebainika kuwa wengi watumiaji wa Sigara na Tumbaku hupata  maradhi ya Kisukari, Kensa,Ugonjwa wa akili na ugonjwa wa moyo.

‘’Tumbaku ni hatari jamani ukiitumia kwa kuvuta ama kwa kutafuna’’ alisema Bi Zuhura.

Amesema kuwa shirika la Afya ulimwenguni limesema zaidi ya watu milioni 8 hufariki dunia kila mwaka ulimwenguni kutokana na matumizi ya tumbaku ambapo kati hao  milioni 7 wanaofariki ni wale wanaovuta ama wanaotafuna.

Ameleza kuwa zaid ya watu Bilioni moja nukta tatu ya wathirika wa tumbaku ni kutoka katika Nchi zenye kipato cha chini.

‘’Sisi Nchi zetu ndio zaid watu wanathirika na matumizi ya tumbaku’’ alisema Bi Zuhura.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa  Zanzibaer mwaka 2011 umeonyesha kwamba kila penye watu 100 watu 7 wamebainika kuwa wanajishuhulisha na matumizi ya Sigara ambapo wengi wao ni wanaume.

Akifungua mkutano huo Afisa mdahini wizara ya Afya, Ustawiwa jamii Wazee  Jinsia na Watoto Yakoub Mohd Shoka amesema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeanzisha Sheria na kanuni ya udhibiti wa matumizi ya tumbaku, Sigara katika maeneo ya wazi ikiwemo kwenye Dala dala, Sokoni na katika sehemu za starehe ili kupunguza madhara yanayotokana vileo hivyo.

Aidha amesema ni marufuku kwa mtu yoyote kuuza, kusambaza kutengeneza, kuonesha tumbaku bila ya kuingiza katika vifungashio maalum ambavyo vinaonesha tumbaku ni hatari kwa afya yako.

Samba mba na hilo amesema kwa mujibu wa sheria na kanuni ni marufuku kwa mtoto chini ya miaka 18 kujishuhulisha na uzaji au ununuzi wa bidha ya tumbaku.

 




 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.