MELI KUBWA LA WATALII KUTOKA UFARANSA LATUA KISIWANI PEMBA.
NA FATMA HAMAD PEMBA. JUMLA ya watalii 69 wamewasili kisiwani Pemba kwa meli maalumu, kwa lengo la kujionea vivutio mbali mbali vya utalii vilivyomo Kisiwani humo. Watalii hao raia wa Ufaransa wamewasili Kisiwani Pemba kwa ziara ya siku Moja, kwa kutumia Usafiri wa meli aina ya LE BELLOT, wameweza kutembelea na kujionea vivutio vya utalii. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwapokea watalii hao, kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alisema ujio wa watalii hao ni kukitangaza kisiwa cha Pemba kiutalii kupitia vivutio mbali mbali vilivyomo. Alisema ujio wao utaweza kuwanufaisha wafanya biashara na wajasiriamali, kuuza na kutangaza bidhaa na biashara zao kimataifa. “Kwa sasa ni wazi kuwa Kisiwa cha Pemba kimeanza kufunguka kiutalii, ujio wao utaweza kuonyesha dunia kuwa Pemba kuna vivutio vingi vya Kiutalii, Pemba ni sehemu salama ya watalii kutembea”alisema. Aidha Mkuu huyo alisema ni meli ya pili hiyo