WALIMU MASKULINI WAHIMIZWA KUJIONGEZA KIELIMU
Afisa Elimu Wilaya chake chake Burhani Khamis Juma kwa niaba ya Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba amewataka Walimu wa skuli mbali mbali kisiwani Pemba kuitumia teknolojia ya mitandao ya kijamii ili waweze kujifunza na kuwafundisha wanawafuzi katika kuleta mabadiliko katika sekta ya Elimu. Afisa Elimu Wilaya chake chake Burhani Khamis Juma kwa niaba ya Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba
Afisa huyo Ameyasema hayo katika hafla ya
kukabidhi vyeti kwa walimu waliohitimu mafunzo ya Elimu
Mtandao na Masafa kutoka taasisi
ya [SHAIBU FOUNDATION ] Chake Chake Pemba .
Amesema kupitia mafunzo hayo ya
elimu mtandao yatatoa fursa kwa walimu kuwajengea
uwezo wa kuitumia mitandao katika kutafuta notis za masomo mbalimbali kwa ajili ya kuwafundishia wanafunzi wao.
‘’Huu ni wakati wa
utandawazi walimu musitumie vitabu tu
katika kuwafundishia ni lazima muitumie mitandao ili muweze kupata vitu vyengine’’ alisema mgeni rasmi.
Sambamba na hilo
amewaasa walimu kuitumia mitandao ya kijamii kwa lengo la kujifunza vitu
ambavyo vitaleta manufaa jambo ambalo litasaidia kuleta ufaulu mzuri kwa
wanafunzi katika masomo yao.
Aidha Akitaja lengo
la kutolewa kwa mafunzi hayo amesema
kwa mujimu wa takwimu na tafiti mbali mbali inaonesha kuwa utumiaji wa mitandao umekua, huku
ikionekana matumizi makubwa yamekua yakitumika vibaya kama vile kuangalia picha
za ngono na michezo ya kamari ambapo mafunzo ya kitaluma yalikua chini.
Comments
Post a Comment