WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA WAPEWA MBINU JUU YA KUPAMBANA NA UDHALILISHAJI WA KIJINSIA.
NA FATMA HAMAD PEMBA. Wasaidizi wa sheria wamehimizwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii ili kuona wanakuwa na uthubutu wa kwenda mahakamani kutoa ushahidi pamoja na kuripoti vituo vya Polisi wakati kesi zitakapotokezea. Hayo yamesemwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Kusini Pemba Richad Mchovu wakati akifungua kongamano la kutimia kwa miaka 10 yautoaji wa huduma wa msaada wa kisheria [Lsf]huko Skuli ya Michakaini Chake chake Pemba. Amesema wasaidizi wa sheria wamekua wakifanya kazi kubwa ya kuibua na kuyaripoti matendo ya udhalilishaji lakini bado jamii inaonekana imegubikwa na tatizo la rushwa muhali. Hivyo amewataka wasaidizi wa sheria kuongeza jitihada ya kuwailimisha wanajamii madhara ya rushwa muhali pamoja na kuwajengea uwezo wa kusimama mahakamani jambo ambalo lisaidia kuondokana na udhalilishaji wa Wanawake na watoto. Kamanda huyo ameahidi kutoa mashirikiano ya hali ya juu kwa wasaidizi wa sheria pamoja na ulinzi shirikishi katika mapambano dhidi ya udhalilishaji ili ku