MUHALI BADO NI TATIZO KWA JAMII
Wananchi wametakiwa kushirikiana na vyonbo vya kisheria kutoa tarifa wakati yanapotokezea matendo ya uhalifu katika jamii ili kuona watendaji wa makosa hayo waweze kupatikana na kutiwa hatiani.
Hayo
yamesemwa na mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kuzuia Rushwa na uhujumu uchumi
Zanzibar Zaeca Ahmed Khamis Makarani wakati akifungua mafunzo ya
siku moja kwa wandishi wa habari juu ya mapambano dhidi ya Rushwa yaliofanyika Gombani Chake chake
Pemba amesema bado jamii inaonekana ikiyafumbia macho matendo ya kihalifu wakati yanapotokezea katika jami
zao.
Amesema
kuwepo kwa rushwa katika jamii ni moja ya sababu inayopelekea kuongezeka kwa
matendo maovu ikiwemo Rushwa, Udhalilishaji pamoja na ujambazi, hivyo basi ni wakati umefika kwa jamii kuacha
muhali na kutoa tarifa kwa mamlaka
husika jambo ambalo litasaidia kuondokana na vitendo hivyo.
Alifahamisha
kuwa kuwepo kwa muhali hakuna maendeleo
yanayopatikana bali hupelekea wanyonge kuonewa na kukosa haki zao.
Nae Afisa
dhamana kutoka mamlaka ya uhujumu uchumi Zanziba Zaeca ofisi ya Pemba Suleiman Ame Juma amewataka
wandishi wa habari kuibua na kuandika habari zinaonesha viashiria vya uhujumu
uchumi uchumi jambo amablo litasaidia mamlaka
ya zaeca kupata taarifa na kuzichukulia hatua za kisheria.
Comments
Post a Comment